GOMASI
Member
- Jan 7, 2011
- 15
- 3
Watanzania tumechoshwa na siasa ya danganya toto, tunataka mabadiliko ya ukweli na sio siasa ya kufurahisha na kunufaisha wachache kama wenzetu wanavyofanya sasa hivi. Kwa mfano kampeni za Tanzania wakati wa chaguzi za viongozi wa taifa utawasikia wagombea wakitoa ahadi kedekede na nyingine zisizowezekana. Kwanza natamani watanzania wenzangu tufikie mahali tuseme sasa basi. Limeibuka jina la ufisadi ndani ya serikali na wahusika kutajwa bila ya hatua yoyote kuchukuliwa dhidi ya hawa wahujumu wa uchumi. Walewale wanaoitwa mafisadi watanzania sijui kwa kulogwa au ni kwa kuhongwa bado wanawapigia kura kuwarudisha madarakani waendelee kuwaongoza. Hivi watanzania kwa fikra hata zisizohitaji elimu, hii ni busara? Tunasubiri nani atuletee maendeleo ndani ya nchi yetu? Mnasubiri wazungu waje kutuletea maendeleo? Ni kweli wazungu wanazidi kurejea Tanzania baada ya kung'olewa wakati wa ukoloni na Mwl. Nyerere. Sasa hivi wanarejeshwa na viongozi wetu kwa jina la uwekezaji. Sawa lakini huu uwekezaji toka uanzishwe umewanufaisha vipi watanzania wa matabaka yote? au ni kuwanufaisha wasaini mikataba na kuwaongezea ufukara watanzania wa tabaka la chini? Kinachonisikitisha zaidi ni pale ambapo chama cha siasa kinaibuka kwa uchungu wa ugumu wa maisha na kuwaelimisha watanzania juu ya ongezeko la ugumu wa maisha, na hatimaye viongozi wetu nyonyezi wanawabatiza jina la" wavunja amani na wachochezi". Hivi hapa wavunja amani na waleta vurugu ni nani kama sio ninyi viongozi mliokatika mshipa wa aibu kila siku mnanyonya uchumi wa taifa kwa faida binafsi? Rais Kikwete ni mara ya ngapi unatajwa kwenye orodha ya mafisadi? Unafikiria nini na dunia inakuchukuliaje? Cha kushangaza zaidi kwenye kampeni za uchaguzi mwaka jana unaonekana unawanyanyua mafisadi wenzako mikono kwamba ni watu safi. Kama kweli wewe ni msafi huwezi kufanya mambo ya kukutia aibu kiwango hicho. Kila siku upo kwenye mikutano na viongozi wa mataifa mengine lakini bado umeshindwa kujifunza kutoka kwao? Wenzako wakishindwa kutekeleza ahadi zao au kutajwa kwenye orodha chafu(black list) kama ufiisadi huwa wanajiuzulu na kuwajibika kwa makosa yao. Bado tu haujifunzi? CCM mmeshindwa kuleta mabadiliko chanya ndani ya taifa letu. CCM mmeng'oka meno aliyowaachia Mwl. Nyerere. Acheni wenye meno ya kutafuna na kupunguza matatizo kama sio kuyamaliza kabisa wachukue hatamu ndani ya taifa letu. Hivi naomba nikuulize JK ulipoingia madarakani sukari ilikua sh. ngapi? Na sasa hivi imefikia sh. ngapi? Bado tu huoni aibu? Yote tisa, kumi mtoto wako Ridhiwani naye sasa ameingia kwenye mtandao wa mafisadi kwa habari za vyanzo mbalimbali. Samahani kama mheshiwa utakasirika, ila inanibidi nikuulize! Wewe ndio mwenyeji wa Ridhiwani ndani mtandao wa ufisadi au ulimteulia mwenyeji mwingine ndani ya huo mtandao wenu? Kweli JK uliingia madarani kwa kishindo lakini unaondoka madarakani kwa aibu kubwa sana.
Langu la msingi naomba watanzania tufumbue macho tuwachague viongozi wenye macho ya kuona matatizo yetu. Viongozi wa sasa wameshafanya matatizo yetu kuwa mtaji wao na ndugu zao.
Langu la msingi naomba watanzania tufumbue macho tuwachague viongozi wenye macho ya kuona matatizo yetu. Viongozi wa sasa wameshafanya matatizo yetu kuwa mtaji wao na ndugu zao.