Kumekuwa na malumbano makali nchini yanayoendelea kwenye vyombo mbalimbali vya habari, hususani mitandao ya kijamii kuhusiana na issue ya Bunge VS CAG
Walio wengi wakiwa upande wa CAG na watu wachache sana wakimuunga mkono Spika Ndugai na Bunge lake, ambalo wabunge wake wengi ni wa CCM
Nami nimekuwa nafuatilia kwa Katibu malumbano hayo, ambayo kwa mujibu wa Spika Ndugai na Bunge lake walishapitisha azimio la kutofanya naye kazi, Profesa Assad na ofisi yake ya CAG
Madai makubwa ya Bunge la Spika Ndugai kutoa azimio lao dhidi ya Profesa Assad ni madai yao kuwa eti analidharau Bunge lao kwa kuliiita dhaifu
Cha kushangaza hata hivyo ni kuwa taarifa za mkaguzi huyo wa serikali, Profesa Assad tayari zishatinga Bungeni na zimeanza kujadiliwa
Ambacho watu wengi tumekiwa tukijiiuliza, je azimio la kutofanya kazi na CAG limeishia wapi??
Nikumbushe kidogo msingi ya utawala bora kuwa kuna Power separation baima ya mihimili 3 mikuu katika nchi, ambayo ni Bunge, Mahakama na Serikali, katika kufanya kazi katika kitu kinachoitwa check and valance
Kwa ninavoona Mimi huu mgogoro uliopo baina ya Spika Ndugai VS CAG, siyo kweli IPO hivyo, bali ninavyoona Mimi mgogoro huu upo baina ya Serikali VS CAG
Huyu Spika Ndugai anatumbikizwa tu hapo kutokana na "remote control" iliyopo pale Magigoni, ambayo inamuekekeza afanye nini
Kama nilivyosema ni kuwa mgogoro huu ni wa Jiwe VS CAG, kutokana na CAG ambaye ni mwakikishi wa Umma wa wananchi wa nchi hii kufanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu na kuonyesha mapungifu makubwa "audit queries" ya serikali hii, ambayo sasa yanatakiwa yajadiliwe Bungeni
Kwa jinsi ninavyoifahamu serikali hii ya awamu ya 5 inavyofanya kazi, haitaki hata kidogo kukosolewa na kuelezwa kuwa kuna mambo hawayafanyi vyema na ndicho kisa chote cha kuinunua ugomvi wote huu na kuigeuza kuwa ni wa Spika Ndugai VS CAG
Imebidi hali ifikie hivyo kutokana na "process" za kumuondoa CAG, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1077, ibara ya/143, kwenye kitu chake kuwa almost to next to impossible!
Ndiyo maana nikasema ni rahisi mno kumng'oa Spika Ndugai kwenye kiti chake cha Spika, lakini ni vigumu mno mithili ya ngamia kupenya kwenye Tundu la sindano, kumng'oa CAG kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu
Mungu ibariki Tanzania