Tunataka kuona mwisho mwema Arumeru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunataka kuona mwisho mwema Arumeru

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by MziziMkavu, Mar 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,609
  Trophy Points: 280
  Vyama ninane ambavyo vimesimamisha wagombea katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru Mashariki viko katika hatua za mwisho kusaka kura kwa wananchi kabla ya kupigwa kura Jumapili Aprili mosi mwaka huu. Wananchi wa Arumeru Mashariki kwa takribani wiki tatu sasa wamesikia kauli za aina mbalimbali za wanasiasa wakijinadi, wakielezea sera zao, wakichambua kwa kina matatizo ya jimbo hilo, lakini pia wakiahidi kuwa

  watazipatia ufumbuzi kama watachaguliwa kuongoza jimbo hilo.

  Kwa ujumla hakuna matukio yoyote makubwa ya uvunjaji wa maadili na kanuni za uchaguzi ambayo yameripotiwa ukiacha malumbano dhidi ya vyama na wagombea wao. Hata hivyo, kumekuwa na viasharia vya kuendesha siasa za ghilba kama vile kughushi nyaraka zinazochafua watu wengine kwa nia ya kusaka huruma ya wananchi katika jimbo hilo.

  Pamoja na hali ya uwanja kutokuonyesha dalili zozote kubwa za kuvunjika kwa amani, tunawajibika kuchukuwa fursa hii kuwakumbusha wadau wakuu katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki kuwa muda wa siku tatu uliobakia wa kampeni ni nyeti sana katika kuufanya uchaguzi huyo kuwa huru na wa haki.


  Ni kweli inajulikana kuwa uchaguzi ni mchakato, kwamba huanza na kujiandikisha wapigakura, kupata wagombea, kufanya kampeni na mwishowe kupigwa kura, kuhesabu na matokeo kutangazwa, lakini katika hatua zote hizi kama hitatawala uchaguzi husika haupati sifa ya kutambuliwa kuwa huru na wa haki. Kwa kuwa kuna siku tatu zimebakia za kampeni, na kwa kuwa kuna suala la upigaji kura, kuhesabu na kutangazwa kwa matokeo,

  tungeomba uvumilivu wa wadau wote katika uchaguzi huu ili mwisho mwema ufikiwe.

  Tunajua kumekuwa na angalizo juu ya idadi ya vituo vya kupiga kura, kwamba huenda vitaongezwa vipya 55 kutoka vya sasa 327, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imesema kuwa kama kutakuwa na haja ya kuongeza vituo itafanyika hivyo kulingana na mahitaji ya wapigakura wanakadiriwa kufikia 127,455; lakini pia ikasisitiza kuwa wadau wote, yaani vyama vya siasa vinavyoshiriki katika uchaguzi huo vitajulishwa kwa maandishi na kwa maana hiyo kushirikishwa vilivyo.

  Tunaelewa kuwa pamoja na hali ya kampeni kuwa ya utulivu wa kiwango cha juu, bado kuna changamoto kubwa sana kwa upande wa Nec katika kuhakikisha kwamba, kwanza; vituo vya kupigia kura vinajulikana, pili; majina ya wapigakura yanabandikwa vituoni ili wapigakura wajue watapiga kura

  zao wapi, tatu; vifaa vyote muhimu vya kupigia kura vinapatikana vituo kwa kiwango cha kutosha na kwmaba utendaji wa maofisa wake unazingatia weledi.


  La muhimu zaidi ni kuhakikisha kwamba kunakuwa na usimamizi wa kiwango cha juu katika vituo vya kupiga kura ili uhuru wa wananchi wa kupiga kura kwa utashi wao, bila shinikizo, bila ghilba au aina yoyote ya kishawishi utimie na hivyo kuupa sifa uchaguzi huo kuwa ulikuwa huru na wa haki.

  Tunakumbusha pia jukumu la askari polisi kwamba wana wajibu wa kulinda usalama katika maeneo yote ya jimbo hilo, polisi wajitambue kama walinzi

  wa uhai na mali za wananchi, kwamba jukumu la kuhakikisha usalama unakuwako Arumeru Mashariki ni lao; wahuni wote na wale wenye nia mbaya ya kuvuruga uchaguzi huo wasipewe nafasi; polisi wakumbuke wakati wote kwamba wao hawafungamani na chama chochote cha siasa miongoni mwa ama hivi ambavyo vimesimamisha wagombea au hata vile ambavyo havikusimamisha wagombea.


  Polisi wanatarajiwa wajionyesha kwa vitendo halisi kwamba wanaongozwa na weledi katika kutimiza wajibu wao katika uchaguzi huo, kwa kufanya hivyo si tu watakuwa wamejijengea heshima kuwa wanajiendesha kwa weledi na hivyo kupata heshima ndani na nje ya nchi, bali pia watapata ushirikiano wa karibu zaidi wa wananchi katika kufichua vitendo vyovyote viovu vinavyochukuliwa au kukusudiwa kuchukuliwa katika kuvuruga uchaguzi husika.


  Ni kwa maana hii tunawaomba basi wadau wote, vyama vya siasa, wagombea wao, wasimamizi yaani Nec, walinzi wa amani yaani polisi, wapigakura kila mmoja kwa nafasi yake, kujipanga vizuri ili siku hizi tatu za lalasalama zimalizike kwa amani na uchaguzi wa Arumeru Mashariki uingie katika kumbukumbu ya kuitwa uchaguzi huru na wa haki.

  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...