Tunasubiri wafadhili kujengewa vyoo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunasubiri wafadhili kujengewa vyoo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chayoa, May 8, 2012.

 1. c

  chayoa Member

  #1
  May 8, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eti watanzania 30,000 wanakufa kila mwaka kwa sababu ya magonjwa ya uchafu, Eti 60% hadi 80% ya watanzania wanaoenda hospitali ni kwa sababu ya magonjwa yatokanayo na uchafu, Na tunatumia Tshs bilioni 301 kwa mwaka kutibu watu hao, kwa hiyo tukope USD 20 Millioni kufanya kampeni ili watu wajenge vyoo na kutumia. Wasichimbe dawa wakiwa safarini, shule ziwe na vyoo vya kutosha, na watoto wetu wajifunze kutumia vyoo, tufanye kampeni watu wanawe wakitoka chooni na kabla ya kula. Za nini hizo si tuwafanye kama kalumekenge, Tunaanza hivi yule mkuu kabisa anatoa amri ikifika cristimas kama kuna mkoa ambao watu wake hawana vyoo basi mkuu wa mkoa huyo ajihesabu kuwa ni mkulima, mkuu wa mkoa naye atatoa amri kwa mkuu wa wilaya, Mkuu wa wilaya naye atatoa amri kwa makatibu tarafa na makatibu tarafa nao watatoa amri kwa watendaji wa kata na watendaji wa kata nao kwa watendaji wa vijiji, watendaji wa vijiji nao kwa wenyeviti wa vitongoji na wenyeviti wa vitongoji nao kwa wasiotakakuchimba vyoo na kuvitumia. Hatimaye kabla ya cristmas mkuu anahitaji taarifa na anaanza kuchukua hatua mbona shule zote kaya zote, na hata wachimba dawa watachukuliwa hatua. hasa kama mahakimu wote wataambiwa akiletwa asiyetakaka kuwa na choo, aliyekutwa anachimba dawa, faini elfu hamsini siku hiyo hiyo au jela miezi sita. Mbona Moshi wamewaweza wachafuzi wa mazingira. TUNAKOPA PESA ZA NINI
   
 2. T

  Tsidekenu Senior Member

  #2
  May 8, 2012
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  this is too much!hadi vyoo!akili zetu zetu ziko wapi?
   
Loading...