AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Hivi karibuni kumeibuka tabia kwa baadhi ya Watanzania wenzetu wasiojitambua kufurahia,kukoleza,kupalilia pale mambo mabaya yanapoikumba nchi yetu.
Mathalani tukio la hivi karibuni la kushikiliwa kwa ndege yetu nchini Afrika Kusini kulikofanywa baada ya mkulima wa kizungu Ndg.Styen kushawishiwa na maadui wa Taifa, kufungua kesi kwa nia ya kumkwamisha Rais wa Tanzania katika shabaha yake ya kulififua shirika la kizalendo la Air Tanzania lililokua limejifia.
Baada ya tukio hilo tumeshuhudia miongni mwetu wakifurahia na kusifu hatua hiyo y kushikiliwa kwa ndege yetu.Hakika huo ni kukosa uzalendo lakini pia ugonjwa wa akili(Psychological Disorder)
Kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kamwe kuthubutu achilia mbali kufurahia nchi yake kupata tatizo hata siku moja.Pamoja na tofauti zetu za kisiasa ,kidini,kikabila linapokuja suala la kitaifa ni vyema wote tuungane n kutetea na kulinda hadhi na heshima ya nchi yetu.
Tabia ya kutaka nchi yetu ikumbwe na mabaya ni tabia mbaya ya hovyo.Sisi ni wamoja tuipende nchi yetu.
Tanzania ikiharibikiwa wote tunakua tumeharibikiwa hatuna nchi nyingine ya kwenza zaidi ya Tanzania.
Tuvipende na kuvithamini vya kwetu.
Augustino Chiwinga