Tunashirikiana na Mashetani kutafuta Rais wa Nchi. Tubadilike tumshirikishe Mungu kupata Rais wa Taifa

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Kuna tofauti kubwa sana kati ya neno nchi na Taifa. Watu wanaoishi nchi ya Tanzania wamekuwa hawajui tofauti ya nchi na Taifa.

Nchi- inahusika na hali ya mazingira,hali ya hewa,ardhi,maji na anga.

Taifa- hawa ni watu wanaoishi katika nchi flani wakaunganishwa kisiasa na kuwa chini ya Serikali moja.

Kiongozi wa nchi huyu hubagua maeneo kwa kuzingatia Dini,Itikadi,Kabila,Rangi au Utashi wake.

Huyu hutafuta sababu mbalimbali za kuhalalisha ubaguzi na upendeleo wa eneo lake.utamsikia matamshi yake na vitendo vyake.huyu hutizama wapi wanaonesha kumpenda au walimpigia kura.na huendeleza sehemu hiyo.

Kiongoz wa Taifa huangalia watu husika.si eneo.huangalia watu wana mahitaji gani.so huangalia hawa watu x wanataka hospital, au shule au barabara. Huyu hukumbuka kuwa watu hao haijalishi walikchagua au hawakumchagua ila anatumia kodi zao.

Huyu hukumbuka watu ,taifa si nchi.nchi haiwez hama.ila taifa linaweza hama.watu ni taifa wanaweza toka sehemu moja kwenda nyingine.si lazima mimi niliyekupigia kura mwaka 2015 mpaka leo naishi pale pale.

Nimeshahama mara nying.what if ntahamia sehemu ambayo hawakukuchagua wewe na umeamua uwakomeshe kwa kutokukuchagua?

Tuepuke viongozi wanaokuwa na roho za kishetani. Za kuwagawa wananchi kwa misingi ya vyama,kabila,dini au kanda.hawa ni waovu kama baba yao shetani alivyo.

Tumshirikishe Mungu...ambaye husisitiza upendo usio na sababu behind.anayesisitiza kumjali na kumpenda anayetupenda na asiyetupenda.
 
Rais ni taasisi inayochaguliwa na wateule wachache sisi ni wawakilishi na kwenye maamuzi hatumo
 
Kichwa cha habari tu kinafaa kupewa 80% ya thread yako.
Bless up
 
Back
Top Bottom