CoolMosi
Member
- Jun 22, 2013
- 50
- 8
Ni siku ya sita sasa tangu j3 ya wiki hii ambapo tulitakiwa kuanza safari ya kutoka Lubumbashi Katanga DRC kuelekea Tanzania,ila tulizuiliwa kwa amri kutoka kwa ofisi ya Gavana kutokana na msururu mrefu wa magari uliosababishwa na askari wa Congo aliempiga risasi dereva wa KiZambia akafa akiwa katika foleni ya kutoka Lubumbashi kuelekea Kasumbalesa Boder Post kisha aingie pande ya Zambia.
Inasikitisha kwani si mara ya kwanza madereva wa kigeni kupigwa risasi ndani ya Congo na Serikali ya Congo haichukui hatua kukomesha hii tabia.
Hali kama hii inatupa taabu sana madereva kutoka Tanzania kwani malipo ni kidogo na pakiwa na tatizo la kuchelewa kama hivi basi wengine huishi maisha ya kuombaomba.
Sasa imesababisha vurugu kubwa baina ya Wazambia na Wacongo hali iliyopelekea kushindwa kwa magari kukatisha Border.