Kwa mara nyingine tena, Spika tulia amezidi kuonesha kwa namna gani alivyo kilaza wa kutukuka.
Leo amewakebehi wanaofurahia Hukumu ya Mahakama ya Rufaa kuhusu Marekebisho ya Sheria yaliyofanywa mwaka 2020 yaliyopoka Haki ya Wananchi kushtaki moja kwa moja kuhusu masuala ya Haki zao.
Alichonisikitisha zaidi Tulia ni kusema kuwa Mahakama ikishatoa hukumu eti wao tena kama Bunge wanaenda kuangalia namna ya kufanya kwa namna wanavyoona wao kama Watunga Sheria.
Kwa mara nyingine tena, nadiriki kusema Tulia Ackson hastahili sio tu kuwa Spika bali hata Daktari wa Sheria kwa sababu anazidi kudhihirisha kuwa yeye ni kilaza wa Sheria na Katiba.
Haiwezekani Spika kushindwa kufahamu kuwa Sheria inapokuwa declared kuwa unconstitutional ni lazima Bunge likienda kurekebisha hiyo Sheria lizingatie maamuzi ya Mahakama kwa kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mahakama ndo chombo chenye sauti ya mwisho kwenye masuala ya Utendaji Haki.
Kusema kweli Tanzania tuna bahati mbaya sana maana vilaza na wapuuzi kama Spika Tulia ndo wanapewa nafasi.