Tunaposema Mfumo Mzima wa serikali Unahitaji Mabadiliko tunamaanisha nini?

marine 1

Member
Jul 29, 2015
60
67
Katiba ya nchi yetu inaeleza vizuri namna ya mfumo wa uendeshaji wa nchi unavyopaswa kuwa.
Katika Uongozi wa juu kabisa kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tz na Makamu wa rais. Kutakuwa pia na waziri Mkuu ambaye ni Kiongoz mkuu wa shughuli za Serikali. Hiyo ni kwa upande wa Muhimili huo. Na jaji mkuu kwa upande wa Mahakama.
Hivyo basi katika mihimili hii miwili ni kwamba kama Rais hatakuwepo, Makamu wa rais atafanya shughuli za rais mpaka atakaporudi. Na ikiwa Rais na Makamu hawapo, basi Waziri Mkuu ataisimamia serikali na kama wote watatu hawapo basi Jaji mkuu ndio atakayekuwa kiongozi wa nchi kwa muda huo.
Hivyo inamaana Makamu wa rais, wazir mkuu na Jaji mkuu wanapaswa kuwa na sifa zisizotiwa shaka zinazomruhusu mtu kuwa Rais kulingana na maelezo ya hapo juu na kwakuwa hawa ni wasaidiz na washauri wa karibu zaidi wa Rais.
Lakini katika hali ya kushangaza katika Mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM, wao wenyewe wameuthibitishia umma kwamba kati ya watu hao watatu (Makamu, Waziri Mkuu na Jaji Mkuu) Hakuna hata mmoja mwenye sifa ya kuwa kati ya watu watano bora kuiongoza nchi ILI HALI WAKIWA BADO MADARAKANI.
Sasa swali ni je nchi ilikuwa kwenye mikono salama, na ukizingatia Rais alikuwa na zaid ya safari 380?
Na je kuporomoka kwa shilingi, ajira, Uchumi,elimu kunatafsiriwaje katika hali kama hii??
 
Back
Top Bottom