tunapong'ang'ania kutumia wastaafu ina maana nchi hii haina wasomi wengine.

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
hv karibuni kumekuwa mijadala juu ya kusimamishwa kazi kwa mgurugenzi wa tanesco bw. mhando na mgao wa umeme unaotarajiwa kuanza hv punde,cha ajabu nilichosikia katika mjadala huo eti generali mstaafu robert mboma ndo mwenyekiti wa bodi ya wakurugezi wa tanesco,ninavyo mfahamu huyu bwana alikuwa mkuu wa majeshi aliyestaafu muda mrefu kidogo inakuaje mtu anastaafu kazi moja anapewa nyingine? jaman mzee huyu amechoka kwanini asipumzishwe kuna watu wengi wenye uwezo na waledi wa kufanya hizo kazi wako mtaani huyu mzee amechuma sana huko jeshini na wengine wapewe nafasi.
 
hakuna haj ya khwa na vyuo nchi hii ,maana hata ukisoma ni sawa na bure kazi hupati ,tunahitaji mabadiliko ya ukweli,wakipe wewe uwaumbue madudu yao watarithi uongozi hadi vitukuu hatukubali
 
Nadhani Watanzania wenye mtizamo huu tunatafsiri kimakosa misemo toka kwenye maandiko matakatifu na methali mbalimbali , mfano aliyenacho ata........na asiyenacho......,Maji hufuata mkondo n,k.Pamoja na kwamba uzoefu wa wastaafu wetu tunauhitaji, naomba iwe inapobidi na sio kubadilisha madaraka ki naman hiii, This is not fair .Kama mnatakaTuondoe ambiquity ya kustaafu kwa mujibu wa sheria basi pelekeni mswada bungeni kwamba mtu astaafu akipenda mwenyewe ili watu muitumikie nchi hii milele mpaka siku mungu atapowaondoa Duniani.Ukisha staafu Kaa pembeni ili kama wataona umuhimu wako basi utaitwa kama mtaalamu mwelekezi(consultant) na sio kurudi kwenye ajira kijanja kama mnavyofanya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom