Somo Zuri -mambo Ya Nchi Za Nje

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
676
Hii nimeitoa Tanzanet. Ina somo zuri toka kwa balozi wa zamani UK. Somo kama hili linaweza kuwa na maana hata hapa JF kama baadhi ya wakubwa ambao wako hapa wangelikuwa na courage ya kuweza kutoa ufafanuzi wa kina juu ya baadhi ya mambo ambayo yanatusumbua wananchi. Soma kuanzia chini (Mimi nilikuwa mpenzi wa Shareef na naamini ni katika mabalozi wachache sana wa nchi yetu ambao utendaji wao ulikuwa mkubwa. I hope huko Ikulu ana kazi ya maana badala ya kupewa desk tu).
---------------------------- Original Message ----------------------------
Subject: Re: [tanzanet]
From: "nawanje99" <nawazinje@yahoo.co.uk>
Date: Thu, June 26, 2008 6:37 am
To: list@tanzanet.org
--------------------------------------------------------------------------

Ndugu Ngalawa

Kusema kweli mimi sina taarifa za undani wa masuala yote mawili uliyouliza. Ila kutokana na taratibu za kidiplomasia na hata kiserikali kwa ujumla wake, nchi X haiwezi kabisa kusema sisi hatumkubali Y kwa sababu yeye si raia wenu!!!!!!!! Ni mwiko kabisa! Uraia wa mtu wa nchi A hauwezi kuamuliwa au hata kukataliwa na nchi B. Hivyo, kutokana na ukweli huo tu wa kisheria, kiserikali, kidiplomasia na hata kiheshima, jibu la swali lako ni wazi. Siyo kweli. Haiwezekani.

Hili la uraia siwezi kukupa jibu maana kwanza sijuwi undani wake na pili ni suala la keshiria na kikatiba; mambo ambayo yote mawili mimi sina utaalamu nayo. Pengine ni suala unaloweza kulipeleka kwa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi au hata kwa Mwanasheria mkuu. Venginevyo, unaweza kumataka mbunge wako aliulize Bungeni ambako bila ya shaka atapata majibu muwafaka kutoka kwa wahusika serikalini.

Ila ningependa kutoa nyongeza ndogo binafsi, kama raia wa Tanzania. Pale niliposikia taarifa kama hizi zilizoeleza kuwa baadhi ya watu wanadaiwa kuwa hawakuwa raia wa Tanzania, nilikuwa Balozi wa Tanzania kule Uiingereza. Shutuma hizo nilizisoma magazetini tu au kuzisikia kutoka kwa wapita-njia. Nilisikitishwa sana na shutuma kama hizo maana baadhi ya walioshutumiwa na kuguswa, kama Ndugu Bandora na Ndugu Ulimwengu, ni watu ambao sote tumekulia na kuwatambua kuwa ni raia halisi wa Tanzania, ambao siyo tu tulifanya nao kazi kuitumikia serikali na Taifa letu la Tanzania kwa miaka na mikaka, bali ni watu ambao walikuwa wakweli, waaminifu, wachapakazi na ambao tuliowasomesha na kuwalea kwa muda mrefu kufika hadi wakawa wataalamu katika fani zao ambazo tumekuwa tukizihitajia kwa udi na uvumba. Ni watu ambao wale waliosoma nao shuleni hadi vyuo vikuu wanawajuwa na kuwatambua kuwa ni ndugu zao Watanzania. Wamekuwa wakitoa michango yao kwa hali na mali kuitimikia Tanzania kwa mika chungu nzima.
Wameshika nyadhifa mbali mbali serikalini. Lakini kufumba na kufumbua -baada ya miaka zaidi ya 40 hivi- kunazuka shutuma eti wao si raia wa Tanzania!!!! Ni raia wa wapi basi?!!!!!Â

Mimi naamini kwamba nchi yoyoote ile dunaini endapo inapata taarifa kama hizo kuhusu watu kama hao wenye ujuzi, utaalmu na uzoefu kama waliokuwa nao akina Ndugu Bandora na Ndugu Ulimwengu, si shani wakataka kuwachukua mara moja na kuanzisha utaratibu wa ama kuwapa uraia WAO, au kutafuta njiya za kuhalalisha ajira yao. Maana ni mfano wa kuokota LULU nchi kavu!
Nani ambaye anajuwa thamani ya "Lulu" aikute nchi kavu halafu aiwache!!!!

Binafsi, mimi naamini kuwa hiyo pengine ndiyo kadhiya iliyomkuta Ndugu Bandora. UNDP waliokota lulu nchi kavu! Waliokota dhahabu barabarani!
Kumbe wafanye nini?!!!!

Ndiyo maana nchi kama Canada na Marekani, ambazo ni mfano wa maendeleo makubwa ya kiuchumi duniani, zimekuwa "zikisaka lulu ncni kavu na kutafuta dhahabu barabarani". Na kila wanapozigundua wanazichota kwa haraka.
Wanaelewa thamani ya "lulu"na thamani ya "dhahabu" katika maendeleo yao.

Sisi Watanzania lazima tukatae tabia za baadhi ya ndugu zetu wenye hulka ya kuzusha fitina na chokochoko za kisiasa ambazo hazina manufaa yoyote kwa Taifa letu na ambzo, wakati mwengine, zinatugharibu thamani kubwa katika maisha ya Taifa letu.

Â
Dr. A. Shareef
Â

--- On Wed, 25/6/08, Jenga Ngalawa <ngalawa@yahoo.com> wrote:
From: Jenga Ngalawa <ngalawa@yahoo.com>
Subject: Re: [tanzanet]
To: list@tanzanet.org
Date: Wednesday, 25 June, 2008, 4:20 PM

Balozi Dr. Shareef,

Shukurani sana kwa majibu yako; kwa hakika binafsi nimepata elimu kutokana na maoni/maelezo yako hapa. Bado nina kaswali kadogo ... inasemekana hapo awali Ndugu Bandora "alipendekezwa" kuwa balozi wetu nchini Ujerumani lakini wajerumani wakakataa wakisema Bandora si mtanzania ... ni kweli ilitokea hivyo au? Baadaye "akavuliwa" uraia wa Tanzania (inaelekea wajerumani walikuwa sahihi) ... baadaye tena "akarudishiwa" uraia wa Tanzania; na baadaye akateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria .... baadaye tena inasemekana baada ya kumaliza "mkataba" wake kule Nigeria, ameamua "kurudi kwao" Rwanda! .... ni nini ukweli wa sakata la huyu ndugu.

shukurani.

jenga


"Knowing is not enough; we must apply. Willing is not enough; we must do." - Johann Wolfgang von Goethe


--- On Wed, 6/25/08, nawanje99 <nawazinje@yahoo.co.uk> wrote:
From: nawanje99 <nawazinje@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [tanzanet]
To: list@tanzanet.org
Date: Wednesday, June 25, 2008, 4:34 AM

Ndugu Edward marahaba!

Mimi mzima na afya yangu na natumai na wewe na wananeti wote mu-hivyo hivyo. Mwenyezimungu awazidishieni.

Ndiyo, kimsingi, nchi moja
inaweza kukataa ombi la kumtuma balozi fulani kwenda kuwa balozi wa nchi yake. Aghalabu, hata hivyo, kidiplomasia, nchi haisemi wazi wazi kuwa hatukubali au hatutaki ujio wa fulani. Kwani ikifanya hivyo, nayo inaweza kufanyiwa vivyo hivyo. Hivyo basi, hutumika njia za kidiplomasia tu "kupeleka"ujumbe wa kutopendezwa na au kutofurahishwa na pendekezo la kupelekwa X Y Z kuwa balozi. Miongoni mwa njia hizo ni kuchelewesha kutoa majibu ya ndiyo. Hapo mwenye akili haambiwi tazama. Atatongoa mwenyewe na kupeleka jina jengine. 99% ya kesi kama hizo, pindi zikitokea, basi husawazishwa kwa njia kama hizo za kidiplomasia: kimya kimya na kistaarabu. Hata hivyo, ni nadra sana, tena sana, nchi fulani kuchukua uamuzi wa aina hiyo. Katika maisha yangu yote ya diplomasia nakumbuka kuwahi kujionea kesi moja tu, mwaka 1991 tena katika nchi ya Kiarabu ambayo ilikataa kusema "ndiyo" au "siyo"kwa mpendekezwa balozi kutoka Marekani. Ilipita zaidi ya mwaka mmoja bila ya kupwa majibu. Kila wakiuliza wanjibiwa tunashughulikia. Marekani walielewa mara moja. Lakini kutoka na kiburi cha ukubwa ilikaza misuli kimyakimya kuanglia kama waombwaji watalegeza uzi. Wapi! Walipoona wanagonga ukuta, na walipbaini kwamba hakuna matarajio ya mmabo kubadilika, wakajisahihisha na kutuma jina jengine. Haikuchukua wiki mbili walipata majibu ya ahlan wa sahlan! Yaani anakaribishwa: "Ndiyo".

Yote hayo yalifanyika kimyakimya na bila ya kusema kitu, si hadharani wala si faraghani. Hapo ndipo mwenye macho haamabiwi tazama na wala mwenye masikio haambiwi sikia. Bali mwenye akili anaambiwa tongoa!

Siyo kweli kwamba
mataifa ya Magharibi au ya Ulaya huwa hayataki kupokea mabalozi kutoka mataifa ya Afrika wenye asili ya jeshi au kutoka jeshini. Wangefanya hivyo wangejikuta katika hali ngumu kabisa pale na wao wanapopendekeza mabalozi wao. Wangekaangwa kwa mafuta yale yale wanayotaka kuwakaanga wengine na hasa kutoka nchi kama Tanzania. Sisi na umasikini wetu hatukubali kunyanyaswa nynanswa kama Taifa. Mwalimu na matukio ya Uwakilishi wa iliyokuwa Ujerumani ya Magharibi kutopendezwa na Uwakilishi wa Ujerumani ya Mashariki ni maarufu katika duru za kidiplomasia.
Aliwashauri wasiopendezwa na uwakilshi huo wafunge virago kama hawapendezwi na uwakilshi huo DSM. Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa Ndugu Yetu Kikwete watafanya vivyo hivyo kwa yeyote yule anayetaka kutunyanyasa hivyo.

Narudia kusema kwamba kukataliwa au kutokataliwa kwa ombi la kutuma mwakilishi kwenda nchi nyengine hakutegemei balozi mtarajiwa anatokea upande gani, bali ni mtu wa aina gani yeye mwenyewe binafsi. Kama mpendekezwa ni mtu anayejulikana kuwa na uhasama binafsi au chuki binafsi na nchi anayotaka kutumwa basi bila ya shaka nchi hiyo itapata ganzi la mdomo kutoa kauli ya ndiyo au siyo. Ikibidi, itatumia mbinu mojawapo ya kidiplomasia, kama hiyo niliyoielezea hapo juu.

Kuhusu Generali mstaafu Kiweru, ninavyoelewa mimi ni kwamba Mheshimiwa Rais alimhitajia zaidi kule Bukoba ambako alihitajika mtu kama yeye mwenye uzoefu mzuri wa ulinzi katika sehemu za mpkani. Utakumbuka kuwa wakati huo hali yetu ya uchumi ilikuwa mbaya kweli, na kulitolewa mapendekezo kadhaa ya kupunguza matumizi. Miongoni mwa mapendekezo hayo ilikuwa kufinga kabisa baadhi ya balozi zetu nchi za nje, mojawapo ikiwa ile ya Ufaransa na Canada [utakumbuka Ubalozi wetu kule Burundi na Rwanda zilikuwa miongoni mwa mapendekzo ya kuzifunga kabisa],, au kuiteremsha hadhi kwa muda kwa kutuma karimu balozi tu na si balozi kamili.

Kwa vile ufungaji wa Ubalozi una athari
kubwa na zinaweza baadhi yake zikawa mbaya, ilipendekzwa kutokufunga Ubvalozi wetu huko Paris na Canada, na badala yake kutuma maafisa wachache tu wa kuendeleza shughuli za kibalozi hadi pale uchumi wetu utapoimarika. Hivyo, Ubalozi wetu Ufaransa ukaiingia katika mkumbo huo; vile Canada, kutokana na uhusiano wetu wa Ki-Jumuiya ya Madola na kwa vile Canada ni mojawapo wa marafiki zetu wakubwa tokea enzi za Trudo, hadhi ya Ubalozi na Balozi iliendelea.

Kwa ufupi ni kwamba Ufaransa haikumkataa Genrali Kiweru, kama unavyosema wewe kutokana na fununu, si kwa kauli bayana wala si kwa mbinu za kidiplomasia, bali ni kutokana na mambo mawili, ninavyo elewa mimi. Mosi uamuzi wa kubana matumizi na kutopeleka Balozi, kwa muda, hadi pale hali itapobadilika, na pili kuhitajika kwa Genrali kumsaidia Mheshimiwa Rais katika eneo la mpakani. Sasa lipi lilikuja mwanza ni shida kusema kwangu mimi. Ila naweza kusema kwamba yote mawili yumkini yalitokea sambamba.Dr. A. Shareef Â

--- On Wed, 25/6/08, Edward Maswanya
<edward.maswanya@postgrad.curtin.edu.au> wrote: From: Edward Maswanya <edward.maswanya@postgrad.curtin.edu.au>
Subject: Re: [tanzanet]
To:
list@tanzanet.org, shareef.abdulkader@gmail.com
Date: Wednesday, 25 June, 2008, 9:01 AM

Balozi Shareef,
Shikamoo habari za siku nyingi ahsante kwa maelezo yako. Naomba kuuliza shwali kidogo.

1.Hivi nchi inaweza kumkataa balozi? kwa mfano Raisi wa Tanzania anamchagua fulani nenda ukawe balozi Ufaranza, halafu Ufaransa ikamkataa balozi wetu? kwa kusema labda mlete mtu mwingine lakini sio huyu.

2.Nasikia kwamba mabalozi wetu wale waliopitia jeshini (JWTZ, JK, Polisi, Magereza etc) huwa hawapelekwi katika nchi za Ulaya bali katika nchi za kiafrika jee ni kweli? kama ni kweli kwa sababu gani?.
Kuna fununu kwamba Maj.General Tumanieli Kiwelu enzi ya uraisi wa mzee Mwinyi alipelekwa Ufaransa, nchi hiyo ikamkataa, ikabidi apaelekwe mtu mwingine. Jee ni kweli ?Naomba maelezo.
Wako
Edward

----- Original Message -----
From: nawanje99 <nawazinje@yahoo.co.uk>
Date:
Tuesday,
June 24, 2008 9:56 pm
Subject: Re: [tanzanet]
To: list@tanzanet.org

> Ndugu yangu Kalala
>
> Sina habari kama Balozi Muganda alifukuzwa kazi!!! Wala sidhani kwamba
> alifukuzwa kazi. Mabalazo wako wa aina
mbili; kuhusu ajira yao. Wapo mabalozi ambao ni wafanyakazi wa
> serikaliwalioajiriwa serikalini kupitia Idara ya Utumishi. Hawa
wanapochaguliwakuwa mabalozi huwa wanaendelea na mkataba wao wa utumishi serikalini,
> hata wanapochaguliwa kuwa mabalozi, hadi kufikia kiwango chao cha
kustaafu utumishi wa serikali. Hawa wanapofika umri wa kustaafu basi wanapaswa kustaafu kama mtumishi yeyote mwengine wa Serikali. Yaani hawa ni wale wanaoitwa: Civil Servants. Karibu miaka mitano iliyopita,
> umri wa kustaafu utumishi serikalini ulikuwa miaka 50 apendapo
> kustaafumapema mtumishi, na miaka 55 anastaafishwa.
Baada ya

> marekibisho,kiwango hicho kilipandishwa kikawa 55 kustaafu kwa hiyari
> na 60 kwa utaratibu wa lazima.
>
>
> Aina ya pili ya mabalozi ni wale wanaoingia mkataba wa miaka mitatu
mitatu au minne. Hawa kila wanapomaliza muhula wao wa miaka mitatu, basi inabidi waache ngazi, ila tu kama wataomba kungezewa muda na Rais
> na Rais naye akakubali kufanfya hivyo. Hivyo basi, kwa mabalozi wa
michapuo yote miwili ya ajira wanapomaliza mihula yao hupaswa kuacha ngazi. Sasa huko si kufukuzwa, bali ni kukamilisha mkataba wa ajira.
Kila mwaka mabalozi kadhaa hukamilisha ajira zao, ambazo ama ni ajira ya kustaafu utumishi wa serikali au kukamilisha mkataba wa ajira, na hivyo hupaswa kuacha ngazi. Naweza kukutajia mabalozi kadhaa ambao wamestaafu:
Balozi Nyanganyi, Balozi Daraja, Balozi Mwawado, Balozi Iddi, Balozi Kateka, Balozi Sarakikya, Balozi Mwambulukutu na wengi
> wengine. Hawakufukuzwa!
>
>
> Â Wakati huo huo mabalozi wengine wapya, wa michapuo yote miwili ya
ajira, waliteuliwa. Miongoni mwao ni Balozi Ngaiza, Balozi Sefue, Balozi Kallegha, Balozi Cisco, Balozi Maharage, Balozi Mwanaidi, etc.,
> etc. Wengine walihamishwa kama Balozi Mwapachu.
>
>
> Kila mwaka mabalozi kadhaa wanastaafu na kila mwaka mabalozi wepya
kadhaa wanateuliwa na Rais. Ndiyo kawaida. Na hali hiyo iko kila nchi,
> si Tanzania peke yake. Ndiyo utaratibu wa kidiplomasia.
>
> Kwa
> matazamo wa haraka, Balozi Muganda lazima amekamilisha moja ya
> michapuohiyo miwili. Kiumri yeye siyo chini ya miaka 60.Hivyo amefikia
> umri wa kustaafu kama walivyostaafu mabalozi wengine kadhaa.
>
>
> Mimi ni mmoja ya wale wanaounga mkono maafisa wa serikali kuacha
> ngazi wanapofikia umri wa kustaafu ili tuwape fursa maelfu kwa maelfu ya
watoto wetu wenye ujuzi, elimu, nguvu ya mwili na akili, utashi, hima na imani kubwa juu ya nchi yao. Maelfu kwa maelfu ya watoto wetu tunaowasomesha kwa hela za walala hoi na baada ya kuhitimu masomo yao tunawatupa barabarani; kwa vile hakuna nafsi za ajira serikalini.Kumbe
> wakongwe wamen'gan'gania madaraka! Siyo sawa! Siyo sahihi! Siyo
busara.Matokeo yake ni kwamba mataifa ya kigeni yanajiokotea
> Wataalamu wetu na
> kufaidika nao. Wataalamu ambao wao hawakusaidia ndewe wala sikio
kuwasomesha! Na wala hatuwezi kuwalamu. Kwa sababu ni sisi wenyweye ndio tuliowatupa "jalalani".
>
>
> Narudia kusema kuwa Ndugu yangu Balozi Muganda hakufukuzwa kazi!
Amemaliza mchapuo wake wa ajira kama balozi. Kama kufukuzwa eti kwa sababu ya ripoti yake kuhusu Zimbabwe basi anfefukuzwa miaka mitano
> iliyopita. Lakini kama sote tunavyojuwa aliendelea kuitumikia
serikali
> yake kwa uaminifu, uzoefu na umahiri mkubwa kule Rwanda hadi kufikia
muhula wake wa kustaafu. Kufikia umri wa kustaafu si kufukuzwa!!!!
>
>
> Nduguyo Shareef
>
> Dr. A. Shareef www.gps-property-maintenance.com Â
>
> --- On Tue, 24/6/08, kalmskys@aol.com <kalmskys@aol.com> wrote:
> From: kalmskys@aol.com <kalmskys@aol.com>
> Subject: Re: [tanzanet]
> To: list@tanzanet.org, shareef.abdulkader@gmail.com
> Date: Tuesday, 24 June, 2008, 8:05 PM

> Balozi Shareef,

> Ahsante kwa uchambuzi na ufafanuzi.

> Swali la ziada:

> Nini kilichomfukuzisha kazi Balozi Muganda kama si hiyo ripoti yake?

> Kama si siri tujulishe ili maelezo yako yapate uthibitisho mzito zaidi.

> Kama ni siri tujulishe ili tuachie hapo hapo ulipotufikisha.
>
> Y. Mtingwa Kalala.

> -----Original Message-----
>
> From: nawanje99 <nawazinje@yahoo.co.uk>
>
> To: list@tanzanet.org
>
> Sent: Tue, 24 Jun 2008 7:54 am
>
> Subject: Re: [tanzanet]

> Salaam Wananeti.

> Nimejikuta sina budi kusahihisha matamshi ya ndugu Emmanuel Muganda
> kuhusu kaka yake na Zimbabwe.

> Ni kweli Balozi
Muganda alihamishwa
kutoka Zimbabwae na kupelekwa
> Rwanda. Ila siyo kweli hata kidogo kwamba alihamishwa kutokana na
pendekzo la aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushsirikiano wa kimataifa, Nd. Jakaya Kikwete. Alihamishwa kutokana na AGIZO la Rais wa wakati huo, Mheshimiwa B. Mkapa. Mimi wakati huo nilikuwa msaidizi mkuu wa Nd. Kikwete pale wizarani na pia Kaimu wake
> nchini, pale alipokuwa nje ya nchi, kikazi. Suala la kuhamishwa kwa
Balozi Muganda nalijuwa vyema. Halihusiani hata kidogo na
> pendekezo wala pingamizi la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Ni suala
linalotokana na AGIZO la Rais. Zaidi kuhamishwa kwa Balozi kutokla kituo kimoja kwenda kituo kengine ni jambo la kawaida.
> Balozi Muganda, ambaye alifanya kazi
> nzuri wakati wake wa ubalozi, hakuhamishwa kutokana na ripoti yake
> aliyoandika kuhusu Zimbabwe. La hasha. Siamini hivyo
hata kidogo.
Ripoti yake ilikuwa safi na ni kuhusu hali halisi nchini,
> kama zinavyokuwa ripoti za Mabalozi wote. Ripoti ilikuwa nzuri na
imesaidia sana kuzidi kuelewa hali halisi ya kisiasa, wakati ule, kule Zimbabwe.

> Balozi anapokuwa katika kituo fulani, huwa ana jukumu la, kwanza
kabisa, kusimamia masilhai ya taifa lake, na pili kuangalia mambo yalivyo katika nchi ya uwakilishi wake na kumuarifu Mheshimiwa
> Rais kupitia Wizara ya mambo ya nje. Balozi Muganda aliandika ripoti
> kiutaalamu kama ilivyokuwa kawaida yake.

> Pili, si busara wala si utaratibu kwa waziri wa mambo ya nje
> kujichukulia mamlaka ya Rais ya kuchagua, kutuma au kuondoa Balozi
katika kituo. Akifanya hivyo, basi si shani kwamba akenda na maji yeye mwenywe; kwani kufanya hivyo ni kumbeza Rais na kumnyanganya madaraka yake ya msingi. Balozi ni mwakilishi
> binafsi wa Rais katika nchi aliyotumwa. Kuendelea au kutoendelea
kumwakilisha katika nchi fulani ni uamuzi wa aliyemtuma
> kumwakilisha. Na anapomtuma kumwakilisha mahali pengine basi ni
kutokana na imani yake kwamba Balozl huyo anaweza kumwakilsha
> vizuri zaidi katika nchi aliyohamishiwa. Lau kama alimwakilisha vibaya
katika nci fulani, basi si jambo la kushangaa hata kidogo kwama Balozil huyo akatimuliwa kabisa katika nafasi ya Ubalozi.

> Ni wazi, kwa hivyo, kwamba Balozi Muganda alihitajika kumwakilisha
> Rais Mkapa nchi aliyohamishwa.

> Ndugu Kikwete hakuhusika ndewe wala sikio na kuhamishwa kwa Balozi
Muganda. Aidha, kuhamishwa kwa Balozi Muganda kutoka Zimbabwe
> kwenda Rwanda hakukuhusika ndewe wala siko na ripoti yake kuhusu hali
halisi
nchini Zimbabwe. Sababu kuu, mimi
naamini, ni kutokana
> na hitajio la Rais kumtuma akamwakilishe mahali kwengine. Na kufanya
> hivyo, bila ya shaka, ni kuonesha imani yake juu ya mtumishi huyo.Â

> Mwisho, siyo kweli hata kidogo kwamba Waziri alishauri Balozi huyo
afukuzwe kazi. Siyo kweli! Waziri hatowi ushauri kwa Rais kuhusu WAWAKILISHI wake, yaani Mabalozi, ila pale tu atapotakiwa afanya hivyo.
Na anapotakiwa afanye hivyo, basi waziri huyu hujumuisha wasaidizi wake wakuu wizarani. Kikwete hakutakiwa kutoa ushauri. Aliagizwa afanye hivyo, kwa sababu nilizozitaja hapo juu. Zaidi, wakti wa kuhamishwa kwa Balozi Muganda, hakuwa balozi pekee
> aliyehamishwa kutoka kituo kimoja kwenda kituo kengine. Mabalozi
> kadhaa
walihamishwa kutoka kituo kimoja kwenda vituo vengine, na mabalozi kadhaa wapya waliteuliwa na Rais kwa minto huo huo.
>

>
>
> Niliona sina budi kusahihisha dhana hiyo ambayo siyo kweli.
>
>
>
>
>
>
>
>
> Dr. A. Shareef
> Â
>
>
>
> --- On Tue, 24/6/08, Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com> wrote:
>
> From: Emmanuel Muganda <emuganda@gmail.com>
>
> Subject: Re: [tanzanet]
>
> To: list@tanzanet.org
>
> Date: Tuesday, 24 June, 2008, 12:04 AM
>
>
>
>
> DM,
>
> That is the problem of Zimbabwe. Robert does not give a damn.
> Lakini na sisi tumemlea.
>
> Once upon a time my brother was an ambassador there. He ( a former
lawyer) wrote a realistic report to our President about Mugabe. Our Foreign Minister did not like the report and suggested he be
> fired. The President
instead transferred him to another country
> and when the foreign minister became president my brother was out of
> a
job. Tumemlea Mugabe.
>
>
> em
>
 
Huyu Mzee hata mimi nilimpenda sana. Alikuwa na msaada mkubwa kwa Watanzania mbali mbali walio nchi za nje hata wale ambao walikuwa nje ya Uingereza. Sasa hivi sijui yuko wapi, mara ya mwisho najua alikuwa naibu waziri mambo ya nje. Ni mwepesi mno kujichanganya na Watanzania wenzake kuchanganua mambo mbali mbali au kujibu maswali yao. Viongozi kama hawa ndiyo Watanzania tunahitaji kuwaweka madarakani.
 
Shareef ni safi na mwenye msada.
Nadhani alipewa Ubalozi wa kweli na siyo kama wale wanaopewa ili walee watoto wa mawaziri na Rais, au wasidie kuhamisha pesa.

Sijui kama mabalozi wengine wanaweza kugeuka na kutojiona miungu. Huko Balozini hawafanyi lolote zaidi ya viburi na kudhani kila anayewafuata anataka kupewa pesa zao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom