Tunapokea kero ambazo ungependa ziwasilishwe bungeni na wabunge wa CHADEMA

Serikali au itoe ruzuku au iondoe VAT kwenye vingamuzi na vocha za digital ili mtanzania wa kipato cha chini aweze kumudu kupata habari kwa njia ya TV.

Serikali ipunguze pay as you earn kwa wafanyakazi kwani kwa sasa ni mzigo mkubwa na inawafanya wafanyakazi wazidi ishi maisha duni kila siku.

Swala la wageni kupata ajira ni kitu cha kuangalia sana kwani sasa kila kampuni utakuta wazungu, wahindi na wakenya wamejaa. Mfano. Kampuni za simu, madini nk. Hii ilikuwa kwenye ilani ya magamba kwamba wangetengeneza ajira lakini haitekelezwi.
 
Tusisahau serikali kufuatilia ubore wa ujenzi wa barabara tenda zinapotolewa. Kwani barabara nyingi kwa sasa zinajengwa chini ya kiwango na hamna anayeuliza. Mfano. Barabara ya chini kutoka bahari beach mpaka mbweni, barabara kutoka segerea mpaka kinyerezi nk.
 
Mkuu wazo lako ni zuri isipokuwa litasababisha maisha kuwa magumu sana kwa watu wa mjini. Kumbuka kuna watanzania wengi tu wanashindwa kulipa hii bili ya maji ya sasa hadi wanakatiwa jumla. Sasa unaposema tena iongezeke si ndo balaa kabisa mkuu. Mi nadhani wasiongeze ila waingizwe kwenye mgao wa hili tozo la sasa, yaani kwenye hili la sasa kuwa na % fulani inayorudi kwenye vijiji husika.
You are very right, hoja yangu kuu ni kuwa wapate pato flan linalotokana na haya maji tunayotumia mijini,nadhan si busara watu wale tukawaacha/kuwatelekeza kama ilivyo sasa. Modality gani itumike ili wawe na gawio la kudumu nadhan wadau wanaweza wakaamua. Aidha naunga mkono suggestion yako kuwa ewura watenge fungu la kuwarudishia watunza vyanzo vya maji na sio yote iishie kwao kwenye kuratibu matumizi ya maji.
 
Huyu si yule dogo wa kibaha au umesahau mkuu?!
Bado anaweweseka kutimuliwa! Uelewa hafifu wa kuzaliwa jumlisha njaa ndio matokeo haya! msamehe tu!
Ni yupi huyo aliyetimuliwa kibaha?? nadhan sina story ya huyu jamaa. Alitimuliwa na chama au raia wenye hasira kali??au ndo huyu mwizi wa simu?? mana naskia hadi kuna wezi wa simu humu.
 
Usimlaumu mwenzio. Hujui kwamba analipwa kwa uvuvuzela huo. Kalaghabaho!
Kazi nyingine ngumu sana. Mtu wa hivi anaweza sema kweli kuwa amechangia chochote katika kuliendeleza Taifa lake?? au ndo anasubiri sisi tuchangie maendeleo ya nchi yeye awe anababaisha hivi???Huyu ashukuru hakuwepo enzi za Sokoine, lazma angeshikwa uzurullaji.
 
Naomba wakashinikize wizara inayoisimamia tume ya uchaguzi/NEC, itoe mwongozo kwa m/kiti wa tume, aweke utaratibu wa kuandikisha/marekebisho watu ktk daftari at least mara 1 kila mwaka. Sio kusubiri mpaka uchaguzi mkuu ukaribie, sababu kila mwaka kuna vjana wanatimiza miaka 18, so mnawanyima haki yao ktk chaguzi ndogo znazotokea, na vilevle kuna watu wanapoteza kadi zao. Nawasilisha!!
 
Sheria ya ugaid ipitiwe upya ili chama chenye mwelekeo huo hususan wa njama za kuua kifutwe kabisa ili kunusuru watu wasio na hatia...
 
Refer proposal aliyoianza Regia Mtema (R.I.P) kwa maana yaliyoongezeka ni muendelezo tu wa yale ambayo hayakuainishwa hapo mwanzo. Nyongeza (japo natoka nje ya maada kidogo) ni viongozi wa juu kujizatiti vyema ili kutoingia tena mkenge wa kuwabariki hawa wenye undumilakuwili/waliokua blinded na ambitions km huyu bwana wa UK.
 
Ewe kijana, nasikitika ya kwamba wewe kama Shonza na Mwambapa kamwe HAMJITAMBUI Hta kidogo katika ulimwengu wa siasa nchini.

Hata hivo siku mkija kujitambua wala hamtokubali kujadhalilisha tena na hizo posho za Tsh 50,000/- mnazoendelea kuzipewa hivi sasa na kusababisha vijana wasomi wazuri tu kama nyinyi hapo KUHIARI KUZIMA SWICHI ZOTE kufikiri japo kwa sekunde moja kwa ajili ya nafsi zenu.

Waache maandamano ya kipuuzi
 
mikataba ifanyike na kupitiwa bungeni huku tukiona na kusikiliza kwenye tv na radio, polisi wasihusike na kutoa vibali vya maandamano ya amaniila wawe wasimamizi wa maandano ili kulinda usalama bila kuingilia maandamano, jaji mkuu asiteuliwe na raisi bali na bunge mikataba yote ipitiwe upya kwa uwazi bungeni, rais asimteue spika wala kuingilia shughuli za bunge .
 
mimi naomba kuuliza maswali mawili

1. kutokana na ujio wa FBI huko Zanzibar naomba kujua ni kiasi gani cha fedha kilicotumika kuwalipa FBI kwa uchunguzi
walioufanya??

2. Kwa mujibu wa CV ya Mhe.Phillip Mulugo naibu waziri wa Elimu alikuwa mwalim kati ya mwaka 2002 mpaka 2004 katika
shule ya sekondari ya southern highland huko IRINGA ilihali hakuwahi kuchukua mafunzo yeyote ya ualimu ktk chuo
chochote hapa nchini kitu ambacho ni kinyume cha sheria za ualimu je Mhe. yuko tayari kulieleza bunge lako kuwa
alivunja sheria za nchi kwa kujiita mwalimu huku akijuwa wazi kuwa yeye si mwalim na je ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya mtu anajita mwalimu huku akijua wazi kuwa hana sifa za kuitwa mwalim??
 
Naomba wabunge wa cdm wakazungumzie issue ya kufungiwa vyombo vya habari kiholela, pia wabunge wa cdm wapeleke hoja mbalimbali bungeni za kuondoa sheria kandamizi katika taifa letu, zinazosababisha ubaguzi wa kichama!
 
tunaomba wawasilishe hili la kungolewa meno na kucha bila ganzi na vijana wa Lwakatare maana kwa sasa linatishia usalama wetu yaan inatulazimu kutembea na sindano ya Ganzi ili ukutanapo na vijana wa Lwakatare ujichome kabisa ili kujipunguzia maumivu
 
Naomba Kiongozi mkuu wa Kambi ya Upinzani(Freeman Mbowe) amuulize waziri mkuu kwenye maswali ya papo kwa papo siku ya Alhamisi nini kuhusu HATIMA ya kesi ya Dr.Stephen Ulimboka kwani serikali ilijitamba sana kwamba ukweli utajulikana na sasa ni miezi kibao imepita umma Haujulishwi kinachoendelea Mahakama isiwe kichaka cha kuchelewesha Haki.

Natanguliza Shukrani!
 
Back
Top Bottom