Ukisoma Biblia
Ezekiel 12-2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.
Haiwezekani unaona kwamba jambo unalotaka kufanya linapingwa na wengi, wa taifa lako na mataifa jirani lakini ukang'ang'ania kulifanya huku ukijua unachofanya hakina afya kwa jamii unayoiongoza! Haiwezekani kwamba unasikia vilio vya jamaa zako wakikusihi kuacha ketekeleza jambao hili wewe ukaziba masikio ilimradi ufanikishe lengo lako hata kama linaghalimu maisha ya wananchi wako!
Rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume na Maalim Seif Sharifu Amad mlifanya kazi iliyotukuka kwa kujenga daraja la amani kati ya Unguja na Pemba na hasa pale mlipobuni serikali ya umoja wa kitaifa. Iliwachukua muda mrefu kutimiza jambo hilo, ingawa si wote walioona thamani yake.
Bahati mbaya, wale wanaoishi katika nyumba iliyoasi wamelibomoa na sasa mahusiano ya Unguja na Pemba huenda yakawa mabaya zaidi ya ilivyowahi kutokea. Gharama ya kujenga daraja hilo sasa itakuwa kubwa zaidi maana sasa nidhahili wapo wasiotaka kusikia kabisa habari ya SUK.
Bado nawashauri wazanzibari wakubali ushauri wa kukubali kuwa na serikali moja ya muungano ambayo naona ndiyosuluhisho pekee la mgogoro uliopo sasa. Mahusiano ya Unguja na Pemba hayatofautiani saana na ya Israel na Palestina. ni Hasi na Chanya, havikutani hata siku moja.
Rais Magufuli, Niwakati sasa wakutengeneza Historia. Anza Mchakato upya wa katiba ya jamhuri ya muungano. CCM wanataka serikali 2, Ukawa serikali 3, yoote hiyo haina tija. Jibu ni serikali 1, hutasikia tena vita ya Urais kati ya Unguja na Pemba, na ninjia pekee ambayo tunaweza kumpata Rais wa Jamhuri anyetoka Pemba Unguja, Kigoma, Tanga, Iringa au popote pale pasipo malalamiko.
Lakini na sisi Viongozi watanzania, kwa sifa yetu tuliyonayo ya amani na utulivu, ya kusaidia kupokea wakimbizi kutoka wananchi waliofarakana katika nchi zao, tuliosaidia ukombozi wa mataifa mbalimbali, tunaoitwa kusuluhisha migogoro yakisiasa katika nchi mbalimbali, hatuoni kuwa tunaelekea kujiaibisha tunaposhindwa kutumia busara katika kutatua migogoro yetu badala yake tukatumia hila, vitisho na ubabe? Tunapo amua kuvunja katiba kwa maslahi ya kundi fulani tunatoa picha gani kwa wanaotutegemea kuwa kimbilio la matatizo yao.
Natoa wito kwamba Hii ya Zanzibar iwe mwisho, na ya Umeya wa Dar es Salaam katu isijaribu kufanana na hii iliyopita.
Mungu ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Amina.