Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,985
- 25,200
Pombe sio Chai tuliipenda wenyewe wacha tuinywe,
Leo pombe ile tuliyoichagua imetulewesha inatupeleka inavyotaka,
ikisema pita huku unapita ,kojoa hapa unakojoa ukijaribu kuipinga ata kidogo inakuyumbisha na kukudondosha,
Pombe ya kwanza kuinywa ilikuwa togwa tuliinywa lakini hatukulewa .
ikaja ya pili tukanywa ulanzi hii tukawa tunalewa huku tunakulana bila kujari tofauti zetu
Pombe ya tatu tukanywa safari hii tukawa tunagonga grass na mashemeji zetu japo kinafiki,
pombe ya nne ilikuwa wine hapo hatukuona aibu kuitoa nje kuinywa ata na majirani zetu huku nyimbo laini ya kusindikiza unywaji wetu zikiendelea kuburudisha nyoyo zetu
Hii pombe ya tano sasa ni Ngumu kumeza inaitwa Gongo ,pombe isiyo na staha ata kwa mashemeji,pombe isiyojua heshima ya wakwe ,
Yenyewe ukishapiga fundo moja inakupeleka inavyotaka
Pombe hii tumeiagiza ndio kwanza tupo grass ya kwanza na imejaa ndoo lakini imeshatulewesha tuko chakali hatuoni mbele wala nyuma tuko hoe hae.
Majirani zetu hawataki kusikia chochote kutuhusu wanatuona maboya kuendelea kuinywa pombe hii inayotuendesha ,
Kuna wanaosema tuiache, wengine wanajifariji kwa kusema uwenda ikapunguza makali kadri tunavyoendelea kuinywa,
na wengine wanasema tuendelee mbona kama inazoeleweka.
Tatizo la pombe hii haitabiliki unaweza kudhani kama imepoa lakini ikiamua kupanda ni kama ina kichaa lazima uwake.