Tunapenda kuhalalisha makosa kwa makosa

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Za asubuhi wana Jf memba

Nikiwa kama msomaji na mfwatiliaji wa mada mbalimbali humu nimegundua asilimia kubwa ya watu humi tunapenda kutumia makosa ya nyuma kuendelea kufaya makosa.

Hii ni baadhi ya mifano kutoka kwenye JamiiForums.

Mada juu ya uchafu Jiji la Dodoma

Ukisoma mule kuna watu wanalinganisha uchafu wa jiji la Dodoma na majiji mengine, mtu anasema mbona hata jiji flani ni chafu, mbona watanzania wote ni wachafu this is totally wrong.

Vita ya Ukraine & Urusi

Kuna watu wanalinganisha vita hii na vita nyingine wanakwambia mbona hata Libya, Iraq, Yemen, Afghanistan n.k watu walikufa kwa hiyo kuna watu wanafurahia watu kufa kisa na huko kwingine watu walimwaga damu.

Hesabu ni janga la Kitaifa/Kimataifa
Hili unakutana nalo shule asilimia kubwa ya wanafunzi wanafeli hesabu kwa kufwata hizi kanuni, mwanafunzi anakwambia kufeli hesabu ni Ishu ya kitaifa so sioni ajabu, na unakuta hafanyi bidii zozote ya kujikwamua.

Mifano ipo mingi sana na siku tutakapoacha kuishi kwenye hizo mentality za kuhalalisha makosa kwa makosa mengine ndipo tutafanikiwa, umeona tatizo flani litafutie suluhisho na sio kujustify kwa makosa mengine.
 
Mkuu; ni hulka ya binadamu kujifunza kutokana na makosa yake au ya wengine. Hapo ndipo utaona umuhimu wa Historia. Bila kutoka nje ya box hutafaulu jifunza vizuri au kuboresha kile kilichopo au Hali/changamoto inayokukabili. Ila ni kufilisika Kimawazo/Fikra na Mtazamo linapokuja suala la kulinganisha pande mbili mbovu halafu ukaridhika na kuona kwamba ah! kwa vile kule nao wanafanya vibaya basi ni Halali/Sawa hata kwako kunapodorora na Kuzembea kutumia ulichojifunza/gundua kama kisababishi na kukigeuza kuwa ni Fursa ya kuboresha au kupambana na Changamoto inayokukabili wewe.
 
Umeme ukikatika kwako unacheki kama kwa jirani upo au la, ukihakiki unajisikia poa.

Tabia ya kishenzi sana hii
 
Back
Top Bottom