Tunapambana vipi na pesa chafu Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunapambana vipi na pesa chafu Tanzania?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by ofisa, Jun 8, 2012.

 1. ofisa

  ofisa JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 1,597
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  NKo safarini kikazi Oman, moja ya vitu walivyonifurahisha ni kureserve maeneo ya kihistoria ukiwemo mji wenyewe wa muscut,
  kuna fly over nyingi na hakuna foleni barabara ni safi na nzuri ila kazi vitu kupata line ya simu lazima uache copy ya passport yako na vitu muhimu. Ukinunua unaulizwa namba ya simu au passport na ninaamini huku Muscat anti-moneylender inapambana kidhati kuliko bongo kila siku semina juu ya hayo hayo
   
 2. M

  MASHAURI RAMADHANI New Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 12, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inakuwa vigumu sana kwa walioko katika nafasi ya kupambana fedha chafu kwa kuwa hakuna alie msafi anaeweza kumfunga paka kengele.

  Jua kuwa kama wewe unafahamu uchafu wangu tunakaa meza moja kutengeneza mikakati ya kupambana na fedha hizo huku ukijua kuwa nyuma ya pazia mimi na wewe ni miongoni mwa watakatishaji wa fedha hizo hiyo mikakati itafanikiwa kweli?.(THOSE WHO ARE IN THE SYSTEM ARE COMPLETELY CORRUPTED THE CAN NOT FIGHT INSTEAD THEY ARE GIVING HAND TO ONE ANOTHER)

  Kwa kuunga mkono usemi ufuatao IF YOU CAN'T FIGHT THEM JOIN THEM.

  Namalizia kwa kusema wanaoonekana ni hawa wadogowadogo wa milion moja mbili tujiulize hivi mikataba tunayoingia ina tija au manufaa kwa Taifa kama si kujaza matumbo ya wachache.THANKS
   
 3. Jodeny

  Jodeny JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo bongo Bro, kila kitu kinawezekana lakini tatizo njaa za wenye mamlaka.
   
 4. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  BRO hakuna pesa CHAFU, huo ni msemo tu, tatizo ni upatikanaji wake BASI, pesa ni pesa haijalishi inapatikana kwa njia gani, Pesa inaheshima jinsi gani unaitumia no matter how you get from. Ni sawa na kusema BLOOD diamond kwa kuwa zinatoka maeneo ya vita na zinatumika kufadhili mauaji, that doesnt make it Not DIAMOND.

  Maendele duni ya Afrika hayatokani na pesa chafu wala Blood diamond, yanatokana na umasiki wa nafsi na roho mbaya za watawala wetu, kila mtu anayeingia katika mfumo wa utawala anataka achote za kwake kisha akajijenge ughaibuni, akishituka muda wake wa kutawala umekwisha na hakuna alililifanya. anakuja mwingine na mambo yale yale.
   
 5. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Mkuu just be honest to yourself...ni mara ngapi umewahi kutumia ofisi yako kupiga dili ukapata non taxable money(hizo ndiyo pesa chafu zenyewe).

  Ikiwa kila mtu anawaza kupiga dili ili awe na RAV 4, Carina, CR-V, Demio etc ya kwendea ofisini ni nani atapambana na pesa chafu.

  Waziri anapiga dili, naibu naye ni mtu wa madili, katibu mkuu(mf Jairo) ni madili kwa kwenda mbele, wakurugenzi hivyo hivyo, maofisa wadogo kadhalika, basi mwisho ni wananchi nao kupiga dili na watoto wetu tunawarithisha maisha ya madili.

  Jiulize kama kesi zilizo wazi kama hizi za EPA, Meremeta zimetushinda ndiyo tutaweza kuwadhibiti wachawi kilingeni wakati tunashindwa kuwashughulikia wakiwa majumbani mwetu....MAWEEEE!!!!

  Anti-Money Laundering inahitaji zaidi ya sheria...MAADILI kama taifa.

  na MAADILI ni zaidi ya kusema tuache wizi, maisha ya watu yawe bora na mifumo iwepo kuhakikisha maisha ya watu ni bora wakati wote..ikiwa leo nipo kazini nanga zinapaa kesho nimestaafu itakuwaje, si ntakufa kwa kihoro na sononeko la moyo...ni kwa muktadha huo naamua kupiga dili ili niwe na uhakika wa maisha yangu baada ya kustaafu.

  nikishapiga dili pesa zangu(dirty money) nazifanyaje??? inabidi nizisafishe kwa kuziingiza katika michakato halali(mf ntajenga jumba nikapangisha na kupata rental income etc) na hiyo ndiyo money laundering.....

  Je, Mkuu unadhani ni vita nyepesi hiyo???
   
Loading...