The Businessman
JF-Expert Member
- Jan 9, 2014
- 7,397
- 9,263
Wana MMU,
Kwa niaba ya familia yetu, nimekuja kuomba ushauri wa kumahauri huyu ndugu yetu Kaka Mkubwa.
Kwa kifupi ni kaka yetu mkubwa ana miaka 37 bado hajaoa na wala hana mtoto, kiuchumi anajiweza kwa kiasi fulani.
Tatizo linakuja ana mchumba "mpenzi" wa miaka 19 na yupo kidato cha 5 na yeye ndio anasema chaguo lake ni hilo.
Kama familia tunaona hilo ni tatizo kwani Msichana alishamwambia asubiri mpaka amalize chuo kikuu ndio waanze mipango ya ndoa kisha kutengeneza Familia.
Kaka yetu kwa wazazi wa bint hajulikani "rasmi" ila bint kwetu familia inamfahamu. Tumejaribu kumshauri atafute bint ambaye yupo tayari kuanza maisha hata sasa kuliko kumsubiria huyu mwanafunzi amalize chuo ndio amuoe lakini imeshindikana yeye amesimamia msimamo wake ule ule anamsubiri bint amalize chuo.
Familia tunaona hilo ni tatizo hasa ukiangalia umri wake ni mkubwa ambao kwa mwingine angekuwa tayari ana familia anayoiendesha.
Wawo kupishana huo umri sisi hatuoni tatizo, tatizo tunaloliona ni kaka kupoteza muda wa kumsubiria bint, na mnajua wachumba wa siku hizi akishafika chuo tu.....kosa.
Bado tunaendelea kumshauri.
Nawe unamshauri nini?