afsa
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 1,986
- 1,585
Rais wangu ananivunjia ndoa kwa mamlaka aliyopewa.
Nimeoa mwaka 2015 nikiwa mtumishi wa umma.
Tangu nioe "Tunda halitumiwi ipasavyo baina yetu wanandoa".
Mwenzangu ameanza kunitishia kutaka kuolewa na mtumishi mwenza anayefanya kazi karibu naye, nahisi tunda sasa linatumiwa.
Mwaka 2016 May nilikamilisha taratibu za uhamisho wa kawaida wa kumfuata mtumishi mwenzangu, uhamisho wa kujigharamia(wa bila malipo), hadi sasa January 2017 haijulikani uhamisho utaruhusiwa lini.
Tangu Rais azuie uhamisho hadi leo Watumishi wote walioomba kuhama ,,uhamisho wao umezuiliwa kwa kisingizio cha uhakiki.
Hakuna mtumishi wa kawaida anayeruhusiwa kuhama hata baada ya kukamilisha taratibu za uhamisho.
Najiuliza ,Rais amesahau? Mbona hataki kuruhusu uhamisho wa wale wanaojigharamia uendelee? Anaogopa nini kwa watumishi wanaojilipia?
Kwa nini mtumishi aendelee kung'ang'aniwa afanyie kazi sehemu ambayo taratibu zote zimemuruhusu akahudumu sehemu nyingine?
Amekusudia kutuvunjia ndoa?
Maswali ni mengi, niishie hapa.