Tunaomba matuta barabara ya Saigoni Kigoma

iqnq

Member
Jan 18, 2021
5
1
Niaje wakuu, mimi ni mkazi wa Kigoma Mjini, kuna hii barabara mpya ya lami ambayo inapita katika mtaa wa Saigoni Kigoma mjini, naomba mamlaka husika zifanyie kazi suala la kuweka matuta katika hii barabara mpya kwa sababu magari na pikipiki zinashuka kwa kasi sana.

Tuna watoto zetu na wake zetu wanavuka wanaenda sokoni na shuleni, tunaomba wahusika waliangalie hili.
 
Msio na magari mnaniuzi sana, hayo matuta yanavunja sana rejeta zangu, jana tu cruser yangu ya mil 75 rejeta imevunjwa.. yaani nyie acha tu
 
Matuta hakuna ila kuna Zebra tatu zebra ya kwanza ipo ile kona ya kuingia legeza mwendo zebra ya pili ipo mitaa ya saigoni uwanjani na zebra ya tatu ipo kule chini kwa nyoka.
 
Back
Top Bottom