Tunaofanya Mazoezi tukutane hapa

masai dada

JF-Expert Member
Dec 29, 2013
15,679
12,362
Mimi sipendi mazoezi ila nimefikia Ile steji ya no way out. Chakula kama chakula kufanya diet au kula michemsho siwezi wenzangu.

Maana kunywa sinywi, club sipendi, starehe yangu ni masotojo tu. Sasa mwili unapoelekea Kwa kweli sio pazuri.

Hii ni wiki ya tatu mfululizo ila napiga ya nyumbani mbio kuzunguka uwanja.
Sit-up sijui ya kukata tumbo. Binafsi naona mwili umeanza kuwa mwepesi.

Naomba kwa wanaofanya mazoezi tupeane ABC please. Vyakula vya kula. Mazoezi ya kufanya na pia tutiane moyo. Binafsi nataka niwe na mwili kama wa Gabu union au tiwa savage nikifikisha 40 bila surgery maana najiona kabisa siwezi kuoitolerate hiyo surgery.

Najilainisha kwanza kabla sijaanza kwenda gym wasije wakanitoa roho bure ma treinaaaa😂😂
 
Matreina watafaidi kuona mtikisiko wa booty 🤣🤣🤣
Piga zoezi kisukari sio poa
 
Yani mazoezi na chakula vinaenda pamoja kwenye kupunguza mwili.

Ukiwa na nidham ya chakula na ukafanya mazoez lazima tu upungue hata km kuna mkono wa mtu.

Punguza vyakula vya sukari, pombe hata sukari kwenye chai, juice n.k kwa kuanzia na uwe na ratiba yako ya chakula na mazoezi bila kukosa.
 
Kwa ndoto ulizo nazo bila kubadili aina yako ya ulaji ni kazi bure mwili mzuri ni chakula health mazoezi ni kidogo sana haya play part kubwa.badili ulaji wako na mazoezi ndo itakusaidia unafanya mazoezi una burn calories kidogo una kula masotojo unaingiza calories kibao waste of time mambo hayo wafanye watu walokolewa na mazoezi haswa miaka washajenga misuli abs six pack hata a kila sotojo anaenda kuzitoa sio mwenzangu na mie utabaki tu mazoezi kwa afya kuwa sijui kama Gaby union tiwa savage sahau.download application za mazoezi zitakusaidia huto hitaji gym maana ni kama trainer tu anakuelekeza anakuhesabia Je unajua english??
 
Walahi hutoboi.Yaani nidham ya kula ndio Kila kitu,mtu ulikuwa una kunywa uji kikombe kimoja ila ukipiga tizi utapiga vinne na Bado unataka upungue,Kwa kweli huo muujiza haupo.
Hapana sili sanaa ila siwezi kufast na kula michemsho nilichoongeza kwenye diet ni natunda mengi na mchicha mwingi na upiga nazi kama yote....so wangapi nimepunguza...napiga nduzi zangu hata mbili au tatu kwa siku au baada ya mazoez au kipindi Cha mlo...alafu mboga kiwango Cha fungu moja napiga nusu...
Siwezi fasting my dear siwezi kula michemsho uwiii
 
Nisaidieni mwenzenu Nina uvivu ila napenda maziez
Anza kufanya chumbani...nunua raba ...Kila saa kumbinna mbili kwenye saa moja tumia dakika 45 au 30 Anza mbio ukishaingia kwenye eqlibrium uwezo lala bila kufanya...
Mimi nilikua na tatizo la usingizi ila now limekata.nalala vizuri hata mchana...nalala.
Jimotivate kwanza mwenyewe utafanya...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom