Tunalishwa mchanganyiko wa sembe na vumbi. TBS, TFDA na serikali mko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunalishwa mchanganyiko wa sembe na vumbi. TBS, TFDA na serikali mko wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jumakidogo, Jul 8, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Haihitaji tume huru, wala uchunguzi wa kina. Hili ni jambo ambalo liko wazi bila shaka hata wanaohusika wanajua. Kumekuwa na idadi kubwa ya viwanda vya kusaga sembe mitaani kisha wanachapisha mifuko na nembo zao wanaingiza mitaani. Sembe ambayo haina ubora kutokana na jinsi inavyotengenezwa katika mazingira machafu. Ukifika Tandale na maeneo ya Manzese shughuli inafanyika bila kificho. TBS haitambui kuwa madukani kuna sembe chungu mzima ambayo haina nembo yao? TFDA hawajui kuwa kuna viwanda vinatengeza vyakula katika mazingira yasiyofaa? Serikali, hasa katika maeneo yanayohusika hawalitambui hili? Au ndio bado mambo yaleyale ya maigizo ya kisiasa?
   
Loading...