Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,018
- 20,489
Kampuni hii inayomiliki hisa 50% kwenye kampuni ya PAP iliyonunua hisa zote za IPTL iliyoliingiza taifa kwenye hasara ya trilioni moja nukta nane hilo ni sehemu ya sababu ya watz kulazimika kuifahamu.
Simba trust imesajiliwa nchini Australia chini ya uwakilishi wa mwanasheria mmoja wa Australia mwenye uswahiba na Tanzania.
Taarifa toka Afrika ya Kusini zinasema Simba Trust imetumiwa na Rais Jacob Zuma kuibia madini nchini Kongo katika kipindi cha vita vya kuwafukuza M23 mashariki mwa nchi ya Kongo, Ndani ya ANC kumeibuka msuguano mkubwa watu wakihoji utajiri wa ghafla wa Rais Zuma tangu kipindi kifupi cha Vitata ya M23,
Taarifa zinasema wizi huo wa madini katika mgongo wa vita vya kimataifa ulizihusisha mamlaka za urais wa nchi tatu ambazo ni Zuma, Kabila na Kikwete, na katika kipindi hicho mpaka sasa, kampuni hiyo haijawahi kulipa kodi kwa biashara hiyo mahali popote katika nchi hizo hali inayotafsiriwa kuwa walifanya hivyo kwa "wizi".
Hapa kwetu tunaona jinsi kampuni hii inavyonufaika kwa wizi huu wa Escrow kwa mabilioni ya umma na nguvu kubwa ya wabunge wa chama tawala kutetea wizi huu. Katika taarifa ya PAC Katibu wa Rais Prosper Mbena ameshiriki kuchota mabilioni ya pesa hizi za umma,
Ikiwa Prospet Mbena amesaini barua kuruhusu pesa zitoke kwa niaba ya raisi huu ni uhusika wa rais yeye binafsi na si kama taasisi, kwani huyu Prosper ni msaidizi wake private.
Kama ingekuwa ni taasisi ya urais tulitegemea Sefue ndiyo asaini, unaweza sasa kutofautisha na kupata picha nia ya ya serikali kuchukua hatua dhidi ya uovu huu ni chafu yenye kulinda maslahi binafsi zaidi.
Tutumie mda wetu kwa maslahi mapana ya taifa letu kuitafuta Simba Trust na umiliki wake na biashara zake hii ni baada ya wale niliowataja wiki juzi kukanusha umiliki huo, ili tujue tunayepambana nae ni nani? isije kuwa ndie tuliyemtanguliza vitani..