Ni vema katika kampeni za uchaguzi huu, hili suala la mafisadi (ambao ndio hao hao viongozi) kutishia maisha ya vijana wa kizalendo wanaofichua ukweli likawekwa wazi kwa wananchi ili wajue kuwa watoto/vijana wao wanaowatetea wako hatarini lakini wenye uwezo wa kulinda maisha yao ni wao wenyewe(wananchi) kwa kupiga kura kuondoa utawala dhalimu unaotishia maisha ya watoto wao. Kura hizo za uchungu zitaleta mabadiliko na usalama wa nchi. Lazima waeleweshwe maana hadaa za CCM sio mchezo.