Tunakoelekea - dunia miaka 25 ijayo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunakoelekea - dunia miaka 25 ijayo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamageuko, Sep 17, 2012.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wadau!

  Nimetafakari hili kwa muda mrefu lakini pia ni vema nikaona tushirikiane katika kufahamishana zaidi. Ukiitazama dunia ya leo tunaelekea katika KUTOAMINIANA, ikiwa zamani watu walikaribisha hata watu wasiwajua wakalala katika majumba yao hata kuishi kabisa leo hii kumwambia mtu alale japo upenuni ni mashaka matupu.

  Hayo ni kwa kifupi katika jamii yetu, lengo langu ni kuzungumzia DUNIA kwa sababu ndio jahazi letu sote, na sote tunafanikiwa tukiwa humu ama kukwama.

  LEO Kila mahala kunajengwa CHUKI, UFISADI, DHULUMA na kila aina za UFISADI, na haitoshi wanaofanya UFUSADI NDIO WENYE KUSIFIWA. Nina khofu sana CHUKI ZA KIBAGUZI zinazojengwa LEO ndizo zitakuwa MAANGAMIZI kwa KIZAZI kinachofuata.

  Nimekumbuka hadithi ya Hannibal mwana wa Hamilcar aliyeishi inakadiriwa miaka 247 – 183 au zaidi kidogo kabla ya kuzaliwa Masihi kwanini namtolea mfano shujaa huyu? Baba yake Hannibal alizoea kumwambia mwanawe juu ya Adui zake (ambayo yalikuwa ni mataifa makubwa wakati huo) hili lilijenga chuki kubwa moyoni mwa mtoto huyo, na hatimae alikusanya maarifa mengi na hatimae kuwa jemedari mkubwa wa vita... Kwanini? Kwa sababu akiona ni vema kufa shujaa kuliko kuishi kinyonge.

  Tusipoangalia NDIKO TUNAKOELEKEA, Leo wako watu kwa makusudi wanaeneza CHUKI kana kwamba wao WATAISHI katika DUNIA hii MILELE. Kesho hawatakuwepo watakuwepo watoto wao je HALI ITAKUWAJE?

  LEO HII YAPO MATAIFA YANAYOONA YANA HAKI ZOTE, Na mengine ni Mataifa Manyonge, je yatakuwa hivyo mpaka lini?

  Leo Idadi ya wabwiaji inaongezeka je vipi ikifika siku hizo HAKUTAKUWA NA WABWIAJI VIONGOZI WA NGAZI ZA JUU?

  JE WAKIZINGUANA NINI KINATOKEA...

  yako mengi mengi mengi ya kutafakari na kujiuliza lakini MIAKA 25 Ijayo....
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kuna uwezekano wakati huo binadamu wakawa wamejirudi na kuwa wema zaidi ya hali ilivyo wakati huu....
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni kweli inawezekana lakini jee? hebu tazama kuanzia WW1 na WW2 waliosababisha walibadilika? Je baada ya WAKOLONI kutupa UHURU wamebadilika? Je wale wageni waliokaribishwa na babu zetu kisha wao ndio wakawa wamiliki na warithi wa babu zetu badala ya wazee wetu wamebadilika? Je siku hizi unaweza kumlaza mtu usiyemjua nyumbani kwako bila kuwa na mashaka (maana yeye atalala wewe mwenye nyumba hutolala, mara ufiche funguo au utafute na makufuli mapya! na hayo ni ikiwa umekuwa na roho ngumu ya kumkubalia kulala hapo!!"
   
Loading...