Tunakijua tunachokitamani?

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Habarini zenu wanajamvi,

Nimekuwa nikifuatilia Post kadhaa bila kuchangia huku nikijiuliza maswali mengi sana,
Watanzania wengi si wakristo si waislamu wameonekana kutamani mno vita yaani mno.
Si wa humu mitandaoni tu bali hata wale wengine ambao nimewafanyia utafiti nje ya
Mitandao.

Sababu zinazopelekea Watanzania kutamani vita ni hizi.

1.Dini
2.Siasa
3.Uchumi mbaya
4.Dhulma.

Sio dhamira yangu kufafanua hayo manne hapo juu, ninachokusudia ni kuwauliza,
kwa sababu nimeshawahi kuishi katika nchi zenye machafuko japo kwa muda mfupi,
Hiyo vita mnayoisikia..... hiyo vita mnayoitamani....... Ikija ndo mtaona tofauti ya
kutazama kwenye TV na pale inapokuwa barazani kwako. Endeleeni kutamani huku
mukikunja ngumi na kuuma meno kwa hasira lakini....................

Tunakijua Tunachokitamani?
 
Maisha yakiwa magumu sana mara nyingi watu huwa hawana cha kupoteza,
Mizinga na mabomu kwao havina nguvu mbele ya dhamira zao zinazosukumwa
na njaa.
 
Mkuu GAZETI, Habari ni salama.Ninatamani haki itawale kiukweli si kwa maneno kwa kuwa ndio msingi wa amani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom