Tunajivunia/tunavumilia kuwa watz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunajivunia/tunavumilia kuwa watz

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Ken Lo, Sep 15, 2011.

 1. C

  Chief Ken Lo Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakuu hii kitu inanipasua kichwa kwa mrefu sana....
  1) naomba mnisaidie katika hili wanajamvi, hivi tunajivunia kweli kuwa wananchi wa hii nchi???kwa lipi???????????
  2)kama tunavumilia kuwa watz, ni sababu gani za msingi zinazotupa huo uvumilivu????
  nawasilisha
   
 2. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tunagawiwa pilau,t shirt,kanga,chumvi,buku tano kila baada ya miaka mitano.
   
 3. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Usiulize Tanzania itakufanyia nini au ikmekufanyia nini. Jiulize utaifanyia nini nchi yako. Hivi is it fair kukaa na kulalamika kila siku kuhusu hii nchi? Ninachoamini,hata CCM wakiondoka madarakani kikaja chama kingine kikatawala. Hakuna mabadiliko makubwa yatakayoweza kutokea iwapo sisi Watanzania hatutakubali kubadilika na kuwa na upendo na taifa hili. Tatizo lililopo ni kuwa tunadhani iwapo chama kingine kitatawala matatizo tuliyonayo yatamalizika. Ufisadi utamalizika iwapo mimi na wewe tutabadilika na kuuchukia. Na matatizo ya kiuchumi kamwe hayawezi kumalizika leo au kesho bali inahitaji sera nzuri na muda pia unahitajika.
  Kwa hiyo Watanzania tunapaswa kuacha ushabiki wa vyama ambao hauwezi kutusaidia lolote.
   
 4. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Binafsi jibu langu ni ndiyooooooooo, najivunia kuwa mtanzania. Natena nina kila sababu ya kujivunia. Ni kweli nchi yetu inapitia kipindi kiguma sana hasa katika nyanja nzima ya uongozi. Jambo hili lisitukatishe tamaa hadi tukaanza kuhisi kama hatuna tene sababu ya kujivunia utanzania wetu.

  Tanzania ni nchi ya amani na pia ni nchi iliojaaliwa rasilimali nyingi sana. Lakini tatizo tulilonalo ni uongozi wetu. Hapa kwa kweli kuna shida sana na inatubidi tuchukue hatua la sivyo taifa letu litaangamia huku twalitazama.

  Wito kwa watanzania wenzangu, chonde chonde tusikate tamaa kiasi hicho kwani hata wazee wetu walipigania uhuru kwa moyo mmoja na wakashinda. Aluta continuaaaaaaaaaaa!
   
 5. msadapadasi

  msadapadasi JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  \

  Mawazo yako ni mazuri ila hoja zako zinapingana na mtazamo wako, ndugu yangu sera za maendeleo ktk nchi zinaandaliwa na kusimamiwa na chama kinacho shika hatamu, so, ili upate sera nzuri ni kwa maendeleo ya nchi ni lazima upate chama chenye sera mbadala na zinazokidhi mahitaji ya nchi hiyo. Hivyo huwezi kukwepa kuwa shabiki wa cha(vya)ma otherwise hujitambui nafasi na umuhiu wako katika kuleta maendeleo ya nchi yako ....
   
Loading...