Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,156
Habari zilizopatikana kutoka nchini Uganda hivi leo ni kuwa Mwanamuziki maarufu nchini humo ambaye pia ni mbunge wa upinzani wa Jimbo la Kyadondo nchini huko Uganda, ameachiliwa huru baada ya kelele nyingi zilizopigwa na vikundi vya kutetea haki za kibinadamu za ndani ya nchi hiyo na kutoka Jumuia ya kimataifa
Tujikumbushe kidogo kuwa Bob Wine na wabunge wenzie 4 kutoka kambi ya upinzani, alikamatwa tarehe 14/8/2018 na kuwekwa ndani na kutakiwa kufunguliwa mashitaka katika Mahakama ya kijeshi kwa makosa ambayo serikali hiyo ya Museveni ilikuwa ikimtuhumu ya uhaini
Baada ya kuwekwa ndani na kutolewa tuhuma za kuteswa akiwa Mahabusu, ndipo vikundi mbalimbali vya kijamii vilifanya maandamano ndani ya Uganda pamoja na nchi jirani ya Kenya, kushinikiza mwanamuziki huyo aachiwe huru
Hatimaye shinikizo hilo linaelekea kuzaa matunda baada ya mwanamuziki huyo kuachiwa huru kwa dhamana na kubadilishwa kwa mashitaka yake badala ya kusikilizwa na Mahakama ya kijeshi, hivi sasa mwanamuziki na Mbunge huyo kijana atafunguliwa mashitaka katika Mahakama za kawaida za kiraia
Je sisi watanzania tunajifunza nini kwa yale yakiyotokea kwa mwanamuziki huyo kukamatwa na kutaka kufunguliwa mashitaka katika Mahakama ya kijeshi na kubadilisha hivi sasa na kumfungulia mashitaka katika Mahakama za kawaida?