Tunajifunza nini katika kisa cha Yusuph

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,520
6,503
Hakika katika matukio ambayo tumesimuliwa katika vitabu vitakatifu yapo mambo mengi ya kujifunza....usisahau popcorn au korosho pembeni yako huku unapata madini!

Jambo la Kwanza ni Usiri katika mambo yako....binadamu sio watu hata kidogo ingawa machoni ni kama watu lkn katika nyoyo zao hakuna utu...na hasa ndugu zetu WA karibu hawa bwana ndio wabaya sana kwakuwa wanajua nyendo zetu na mipango yetu....wanasema kikulacho kipo kinguoni kwako hakika wahenga hawakukosea kabisa...kuna watu wetu WA karibu hawapendi mafanikio yetu...hawapendi kuona tunatoka sehemu moja na kwenda level nyingine kimaisha na furaha Yao ni kutuona daima tunataabika na kupata shida...kwahiyo sio kila Jambo la kuongea nao...mambo mengine weka Chini ya kapeti wayaone Tu yakiwa yameshakamilika.

Rejea katika kisa cha Yusuphu...alimwambia Baba yake hakika Mimi nimeona ndotoni Nyota Kumi na moja pamoja na Jua na Mwezi vikinisujudia...mara baada ya kumwambia Baba yake hiyo ndoto yake...Nabii Yakubu alimwambia mwanae...usiwasimulie hiyo ndoto yako hao ndugu zako kwani hakika shetani ni adui dhahiri Kwa binadamu....hapo tunaona kabisa kwamba Nabii Yakubu aliogopa wasije ndugu zake wakaingiwa na fitina na kumdhuru ndugu Yao....nitanukuu Aya ya Qur'an :
Suratul Yusuphu
إِذْ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَا أَبَتِ إِنِّي رَأَيْتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوْكَبًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ رَأَيْتُهُمْ لِي سَاجِدِينَ

Yusuf alipo mwambia baba yake: Ewe babaangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua, na mwezi. Nimeota zikinisujudia.


قَالَ يَا بُنَيَّ لَا تَقْصُصْ رُؤْيَاكَ عَلَىٰ إِخْوَتِكَ فَيَكِيدُوا لَكَ كَيْدًا ۖ إِنَّ الشَّيْطَانَ لِلْإِنسَانِ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui aliye dhaahiri kwa mwanaadamu.


Jambo la pili...Tusionyeshe upendeleo katika kuwapenda watoto wetu....hakika Nabii Yakubu alionyesha mapenzi yake makubwa Kwa Yusuphu na Kaka yake....mpaka ikawapelekea wale ndugu wengine kuona wivu na hivyo kutaka kumdhuru Yusuphu au kumuua ili mapenzi ya Baba Yao yawaelekee kwao...hata Sisi huenda tukawapenda baadhi ya watoto wetu kuliko wengine,au mtoto mmoja badala ya mwingine...hii huweza kutokea huenda kutokana na Tabia ya mtoto husika ikakupendeza na hivyo ukajikuta unampenda zaidi ya mwingine...lkn pamoja na yote hayo basi tujitahidi kubalance upendo ili huyo mwingine au hao wengine wasione kabisa wazi wazi kuwa tunabaguliwa....kwani hiyo Hali yaweza pelekea kuleta uhasama miongoni mwao:
Rejea tena ktk Suratul Yusuphu

إِذْ قَالُوا لَيُوسُفُ وَأَخُوهُ أَحَبُّ إِلَىٰ أَبِينَا مِنَّا وَنَحْنُ عُصْبَةٌ إِنَّ أَبَانَا لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

Pale walipo sema: Hakika Yusuf na nduguye wanapendwa zaidi na baba yetu kuliko sisi, hali sisi ni kikundi chenye nguvu. Hakika baba yetu yumo katika upotofu wa dhaahiri.

اقْتُلُوا يُوسُفَ أَوِ اطْرَحُوهُ أَرْضًا يَخْلُ لَكُمْ وَجْهُ أَبِيكُمْ وَتَكُونُوا مِن بَعْدِهِ قَوْمًا صَالِحِينَ

Muuweni Yusuf, au mtupeni nchi mbali ili uso wa baba yenu ukuelekeeni nyinyi. Na baada ya haya mtakuwa watu wema.

Jambo la tatu....Hakika Mwenyezi Mungu ndio mwenye mipango Bora kabisa.....tunaona kuwa baada ya ndugu zake Yusuphu kutaka kupanga mpango wa kumuua...lkn bahati nzuri miongoni mwao akasema msimuue Ila mtupeni katika kisima baadae watakuja wasafiri na kumchukua na kuondoka nae....na kweli walimuingiza kisimani...lkn Nabii Yusuphu akapewa maono na Mwenyezi Mungu IPO siku utawasimulia hii habari nao hawatambui:


فَلَمَّا ذَهَبُوا بِهِ وَأَجْمَعُوا أَن يَجْعَلُوهُ فِي غَيَابَتِ الْجُبِّ ۚ وَأَوْحَيْن إِلَيْهِ لَتُنَبِّئَنَّهُم بِأَمْرِهِمْ هَٰذَا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ

Basi walipo mchukua na wakakubaliana wamtumbukize ndani ya kisima, tulimfunulia Yusuf: Hapana shaka yoyote utakuja waambia kwa jambo lao hili, na wala wao hawatambui.

Na kweli walikuja watu kuchota maji kisimani wakamtoa kisimani na kwenda kuumuza huko mbele ya safari...kwahiyo huenda wewe umetumbukizwa kwenye majanga mbali mbali,huenda umedhulumiwa,unamnyanyaswa na mapitio yote magumu unayopitia lkn kumbuka Mwenyezi Mungu atakutafutia njia ya kutokea kama Yusuph alipotoka ndani ya kisima kile.

Jambo la nne...Mwenyezi Mungu pekee ndo awezaye kutuepusha na machafu na maovu..Nabii Yusuph baada ya kuuzwa huko Misri..alinunuliwa na bwana mkubwa mmoja kiongozi ktk hiyo serikali...akamwambia mkewe naona tumchukue huyu kijana huenda akatufaa huko baadae au tukamfanya kuwa mwenzetu...sasa Yusuph inasemekana alikuwa hand some Sana yaani hakuna binadamu wa kiume mzuri kama yeye...kwahiyo alipofikia ukubwani mke WA Waziri alimtamani Yusuph Bila ridhaa yake...lkn tunaambiwa Yusuph nae angelimtamani pia Lau kuwa Mwenyezi Mungu hakumuonesha ishara...na Mwenyezi Mungu anasema hakika Yusuph alisafishwa nafsi yake na mambo maovu:
Rejea ktk Suratul Yusuph tena...




وَلَقَدْ هَمَّتْ بِهِ ۖ وَهَمَّ بِهَا لَوْلَا أَن رَّأَىٰ بُرْهَانَ رَبِّهِ ۚ كَذَٰلِكَ لِنَصْرِفَ عَنْهُ السُّوءَ وَالْفَحْشَاءَ ۚ إِنَّهُ مِنْ عِبَادِنَا الْمُخْلَصِينَ

Na hakika yule mwanamke alimtamani, na Yusuf angeli mtamani lau kuwa hakuona ishara ya Mola wake Mlezi. Hayo hivyo ni kwa ajili tumuepushe na uovu na uchafu. Hakika yeye alikuwa katika waja wetu walio safishwa

Kwahiyo hapa tunaona Bila rehma ya Mwenyezi Mungu ni vigumu Sana kwetu Sisi kuepukana na maovu na machafu...kubwa turejee Kwa Mola wetu tutubu na kumuomba atuongoze katika njia iliyonyooka ili tupate radhi zake na muongozo wake.

Jambo la Tano...Mwenye kufanya dhuluma hatengenekewi.....baada ya mke wa wazir kumtaka Yusuph kinguvu..ilibidi Yusuph akatae kwakuwa aliona amekirimiwa vizur na mume wa Yule bwana pale na kumpa makazi mazuri iweje amdhulumu Kwa kutembea na mke wake.


وَرَاوَدَتْهُ الَّتِي هُوَ فِي بَيْتِهَا عَن نَّفْسِهِ وَغَلَّقَتِ الْأَبْوَابَ وَقَالَتْ هَيْتَ لَكَ ۚ قَالَ مَعَاذَ اللَّهِ ۖ إِنَّهُ رَبِّي أَحْسَنَ مَثْوَايَ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ

Na yule bibi wa nyumba aliyo kuwamo Yusuf alimtamani kinyume cha nafsi yake, na akafunga milango. Akamwambia: Njoo! Yusuf akasema: Audhubillahi! Najikinga na Mwenyezi Mungu. Huyu bwana wangu kaniweka maskani nzuri, na hakika wenye kudhulumu hawatengenekewi.

Hapo tunaona kuwa hata kutembea na wake za watu ni dhuluma.....je ni wangapi wanatembea na wake za watu? Na kibaya Zaidi mpaka wengine mnazaa nao kabisa...je hamuoni kuwa mnawadhulumu hao waume zao? Hakika anayedhulumu hafanikiwi...huenda sio kimaisha lkn Mola wako anajua zaidi.

La Tano ni....Umuhimu WA kuwa na Subira....hakika ktk habar ya Yusuph kuna mambo mengi Sana ya kujifunza...Mimi Kwa muktadha wa Uzi huu nimechambua machache....baadae Yusuph alipelekwa gerezani na kukaa Miaka kadhaa..baadae alitoka baada ya mfalme kumuhitaji kutafsiri Ile ndoto aliyoota mfalme...ambapo mfalme aliota kuwa...ng'ombe Saba wanene wanaliwa na ng'ombe Saba waliokonda na mashuke Saba mabichi na mengine makavu....sio lengo langu kuelezea hii ndoto...lkn kwakuwa Yusuph alifundishwa na Mola wake kutafsir mambo basi aliitwa na kuitafsir Ile ndoto...na baadae likasafishwa Jina lake kutokana na Ile kashfa ya kusingiziwa kumtaka mke wa wazir kinguvu,kumbuka baada ya mke wa wazir kumkimbiza Yusuph..wote walikimbilia mlangoni na kukutwa pale mlangoni na Waziri, ndo mkewe akamsingizia Yusuph kuwa alitaka kumfanyia maovu...kwahiyo akaonekana hakuwa na hatia na baadae akaja kuwa mmiliki wa hazina zote pale Misri...hapa tunajifunza hakika Maisha Yana mapito mengi...kuna milima na mabonde lkn mwisho mwema huwa Kwa wenye Subira..

Ni hayo Tu.
 
Huu Uzi inaelekea maadmin wanaufuta...nimetuma zaidi ya mara nne...sijui cha ajabu ni nini ktk huu uzi
 
Duh! kumbe ulifutwa labda moderator leo yuko ndugu yake Maghayo
Ulifutwa Kaka....kuna wkt nilifikiri nimeufuta bahati mbaya...nikapost tena ukaja ule wa mwanzo hlf ukapotea...nikatumia tena ukapotea...ndo Nataka wafute mara ya mwisho nijue hautakiwi
 
Ulifutwa Kaka....kuna wkt nilifikiri nimeufuta bahati mbaya...nikapost tena ikaja ule wa mwanzo hlf ukapotea...nikatumia tena ukapotea...ndo Nataka wafute wafute mara ya mwisho nijue hautakiwi
Hongera sana kwa kuwa na moyo wa kuandika tena ,mimi uzi ukifutwa mood ya kuandika tena sina kabisa.
 
Hongera sana kwa kuwa na moyo wa kuandika tena ,mimi uzi ukifutwa mood ya kuandika tena sina kabisa.
Bahati nzuri niliuandika pembeni kwahiyo nauhamisha Tu.....yaani nikitaka kupost na copy na kupaste tu
 
Huyu admin atakuwa mvulana Tu ....kama namkera anifute kabisa...maana huu ni upuuzi!
 
Ma shaa allah , .kisa cha yussuph kina mafundisho makubwa mno mpka Allah anamuinua, kisa hiki hakikua ni hadithi tu zitufurahishe ila tupate mafunzo juu yake.
Allah akuhifadhi
Shida wanauweka huku uzi hauwafikii wengi. Nashindwa kuelewa lengo la jf kweny jukwaa la dini ni kwa watu wachache tu au laa
 
Hii hamjaicopy kutoka kwenye Biblia?
Ukipata muda soma Biblia, Mathayo yote jinsi Yesu alivyozaliwa mpaka kufa na kufufuka halafu soma Quran kwa Issa. Yesu na Issa ni mtu yule yule?
 
Ma shaa allah , .kisa cha yussuph kina mafundisho makubwa mno mpka Allah anamuinua, kisa hiki hakikua ni hadithi tu zitufurahishe ila tupate mafunzo juu yake.
Allah akuhifadhi
Shida wanauweka huku uzi hauwafikii wengi. Nashindwa kuelewa lengo la jf kweny jukwaa la dini ni kwa watu wachache tu au laa
Ni mtihani Sana kwakweli ukhty
 
Huu Uzi inaelekea maadmin wanaufuta...nimetuma zaidi ya mara nne...sijui cha ajabu ni nini ktk huu uzi
Hawa maadmini mda mwingine sijui wakoje aisee
Wakiona nyuzi za waislamu tena zina mafundisho mazuri tu wanazifuta ila sasa za upande wa pili tena wanaudhihaki Uislamu na hazifutwi
Inshort wanayumba kwenye hili
 
Mm wamenizuia kuuona uzi nilouandika mimi mwenyewe
Uzi una kichwa cha " Zinduka ndugu yangu muislamu" ila naona tu likes ila m nikiufungua haufunguki sasa sijui wanashida gni hawa maadmini
 
Hii hamjaicopy kutoka kwenye Biblia?
Ukipata muda soma Biblia, Mathayo yote jinsi Yesu alivyozaliwa mpaka kufa na kufufuka halafu soma Quran kwa Issa. Yesu na Issa ni mtu yule yule?
na wewe ukipata muda pitia kitabu alichotumia mtoa mada...
 
Jf sio kanisa Wala msikiti. hizo porojo zenu kapigianeni huko mnako jazana ujinga Kama Ni msikitini huko huko Kama Ni kanisani huko huko msitusmbue
 
Mm wamenizuia kuuona uzi nilouandika mimi mwenyewe
Uzi una kichwa cha " Zinduka ndugu yangu muislamu" ila naona tu likes ila m nikiufungua haufunguki sasa sijui wanashida gni hawa maadmini
Nimeuona jukwaa la dini
 
Back
Top Bottom