Tunajifunza nini juu ya kesi ya Prof. Assad?

Assad hakumuonea mtu, kilichomponza Ni kusema ukweli na kufukunyua madhambi ya gvt
 
Unajua maana ya kiapo cha SITO TOA SIRI?

sasa Kwa mfano mtu anataka kuhatarisha usalama wa taifa zima unataka bado awepo Tu just because akitolewa katiba inavunjwa?

Kuna mambo mengi zaidi viongozi wanafanya Kwa ajili ya manufaa ya wanainchi
usalama wa taifa kwa kuhoji zailpo trilion 1.5 ? kwani Asad alifanya nini zaidi?
 
Mahojiano yake kule New York niliyasikia vizuri tu. Na ndicho kilichowakera wanaojiona wenye nchi. "IKIWA SISI (CAG) TUMEONYESHA UBADHIRIFU SERIKALINI NA HATUA HAZIKUCHULIWA BASI UTAKUWA NI UDHAIFUWA BUNGE" Kwani sisi kazi yetu ni kuionyesha bunge, na bunge ndiyo inaichukulia hatua serikali kikatiba. Sasa hapa kosa la Asad lilikuwa wapi ?!

Na kama ni hizo fedha za kitengo ndiyo ilikuwa ni tatizo. Ujue ndiyo kichaka cha ubadhirifu. Kutumia kodi za wananchi bila kulitolea maelezo ni ufisadi ule ule. Kitengo lazima kiwe adilifu ili kutoa mfano. Siyo kichaka cha kufichia matumizi mabaya serikalini.
 
Hivi unahisi kama asingekuwa allah kuingilia kati haki ya assad ingepatikana leo??
 
What if 1.5 zilinunua vifaa vya jeshi?

Kwani ni lazima yy ambiwe? But magu sio mjinga amtoe Kwa kuhoji 1.5 lazima kuna kitu na sio muhimu Sisi kujua, as long as mambo yameenda vizuri
Kosa lako ni kuamini watu badala ya katiba. Watu ni viumbe hai huja na kupita . Kama zilivyo tawala nazo huja na kupita. Lakini katiba ipo kwa masilahi ya taifa siku zote za uhai wa taifa husika.

Mfano leo yuko wapi Maghufuli, lakini Tanzania ipo na katiba ipo. So mapenzi yasikupofushe ukaiacha kweli.
 
Sometimes kiongozi anavunja katiba Kwa Benefits za watu wengi so hakuna shida

Sidhan kama magu alimtoa bila kosa, lazima kulikuwa na makosa

And possibly yangegharimu uongozi wake and sio kila kitu cha kutolea maelezo Kwa wanainchi
Hao wawili walikuwa chui na paka, Assad alianza kumponda Magu toka Magu hajawa rais mara ghafla Magu kawa mkuu wa nchi.
 
Kwa hiyo unaamini sasa umuhimu wa kuwa na Katiba mpya? Mwalimu Nyerere aliliona siku nyingi hili kuwa katiba hii inampa Rais umungu mtu.
 
Hao wawili walikuwa chui na paka, Assad alianza kumponda Magu toka Magu hajawa rais mara ghafla Magu kawa mkuu wa nchi.

Kwa kibongo bongo kukomoana lazima so no problem haha haha
 
Magufuli alikuwa na uchungu kweli na maendeleo ya hii nchi. Shida ni pale alipoamini kuwa ni yeye pekee alikuwa anajua kila kitu. Ule ulikuwa ni ubinafsi.
Magufuli hakumfukuza kazi Asaad. Alichofanya ni kutokumpa mkataba wa pili pale mkataba wa kwanza ulipoisha. Na sheria ya National Audit Act ilimruhusu Magufuli kufanya hayo. Na hiyo sheria ilitungwa na kupitishwa kabla Magufuli hajawa Rais wa JMT. Walichosema High Court ni kwamba hiyo sheria inapingana na Katiba. Hapo Magufuli kosa lake ni lipi? Hiyo sheria hakuitunga yeye mbona?
 

Hawa si wazee wa uchawa? Hawawez kujua hayo mambo
 
Assad anaamini yeye yupo sahihi kuliko wengine wote, alijiona yeye ni kama boss wa nchi nzima kwa hiyo nafasi ya kuwa CAG, na kama nae angekuwa rais pengine angekuwa ni majanga zaidi na mwisho Assad nae ni mtu wa visasi.
 
Jitu kwa kukosa maarifa linamtetea Magufuli, tuonyeshe basi kivipi hakuvunja katiba- hawezi. Eti oooh mzalendo, wapi pameandikwa ukiwa mzalendo ruksa kuvunja katiba
Kwani katiba ni msaafu?? Kwamba hata angemtukana rais basi aangaliwe tu sababu kuna katiba?

Nafasi yake ilikuwa finyu kuliko nafasi ya urais ya mwenzie. Akitaka achukue fomu 2025 kama rahisi.

Huyu alianza kutofautiana na Magufuli pale ofisi yake ilipopunguziwa bajeti.Akaanza kusema atashindwa kuwapeleka vijana wako nje kusoma na kuchukua mafunzo. Hapo tayari kila ofisi ilipunguziwa bajeti ya safari, warsha, posho na vikao. Wakati ye anaona kisima mwenzie alikuwa anaona bwawa.

Kuongezea juzi mama kasema mtu akimpinga hatoshirikiana nae, na hata sheria za nje zikimbana yeye atatumia kanuni zake kuwabana. Ndivyo ilivyo.
 
Magufuli tabia zako ulizoishi hapa duniani sasa unazalilika sana kila ulichofanya kibaya kimetinduliwa wakiwemo vibwengo wako mapunda na clock bad.
Kuzuia mikutano ya kisiasa kwa wapinzani mbona Samia kaona ni jambo zuri kutoka kwa Magu.
 
Sometimes kiongozi anavunja katiba Kwa Benefits za watu wengi so hakuna shida

Sidhan kama magu alimtoa bila kosa, lazima kulikuwa na makosa

And possibly yangegharimu uongozi wake and sio kila kitu cha kutolea maelezo Kwa wanainchi
Hii kali kidogo kumeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…