Tunaitoaje CCM madarakani?

1.Majuzi tu vyama vimeungana kuifungulia kesi serikali mahakama ya africa Mashariki kupinga sheria ya vyama vya siasa pia ukawa bado unamshikamano

2.Kwa haya mazingira ya kukataza vyama vya siasa kufanya mikutano ingawa ccm wanafanya,kunyima Uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari,kuwafunga na kuwashambulia wapinzani mfano lema,sugu, Mbowe na lisu.Kwa mazingira haya watajitangazaje? Kule Zanzibar ccm hawajawahi kushinda,Maalim anajulikana zaidi ya magu.
 
Umechambua vizur sana mkuu. Nakupa heshima ya juu. Nakubaliana na ww kwa mengi uliyobainisha.

Nianze na point yako. Tumtoe CCM tumuweke nani. Kwa kweli kwa Sampuli ya wapinzani tulionao inatupa walakini. Ukiwatazama kwa jicho la ndani utawaona kua hawatetei watz bali mlo. Ndo maana ni wadhaifu wananunulika. Na wanashutumiana wao kwa wao. Mtu ajiitae Yeriko kada mtiifu anawakilisha yaliyomo chumban Chadema siku alivyokua anawaponda ACT kisa ti wamepata wafuasi wengi. Yaani wakachukia kitendo hicho. What a shame Yeriko.

Mbowe.

Mbowe ni Mungu mtu CHADEMA. Hashauriki, hapingwi, hakosoleki. Ukifanya hivo ujue njia ya ya kuondoka Chadema ni nyeupe. Hakika anawafanya Watz wawaone chadema kama Fisi mmwenye njaa kali awezaye kula matumbo yake mwenyewe. Anadaiwa kuteua VITI MAALUMU kwa upendeleo ikihusishwa na ngono. Juzi ulimsikia polepole alivokua anatuma vijembe na yule mama kule bungen alivokua anajitetea. Baadhi ya watu huona bora fisi alie shiba kuliko mwenye njaa alae matumbo yake ( chama chake).
Kiukweli Mbowe sio mtu wa kukabidhi nchi.

Zito na ACT yake.

Huyu ni kijana mzalendo na mwenye kujiamini na mbwiba mkuu kwa serikali. Lakn namuona kama ni mtu ambae ana chuki na wapinzani wenzie (Chadem) kutaka hata kulipiza kisasi. Ndo maana siku za nyuma wapinzan wote walitoka bungen ila yy tu na pia kutojiunga na ukawa ndo ikawafany watz waahisi pengne wengn kuamin kua ACT ni CCM B. Na pia sidhan kama Zitto anaweza achia ngazi cheo chake chaman...yaleyale ya Mbowe
Hii inaondoa jitihada za kuitoa ccm madarakan.

Nini kifanyike?

Twahitaji wapinzani imara, mathubuti na wazalendo wenye kujiamin. Sio hawa tulio nao akina Mbowe, kubenea, etc. Watu ambao ukiamka utataka uskie ni nan ambae ameunga juhudi kwa siku hio. Ni watu wenye njaa kali, asie tabirika. Tumahitaji watu wa aina ya MALEMA wa Africa kusini. Watu wa kujitoa walio tayari kufa kwa ajili ya wengne.

Twahitaji pia watu waamke kuutafta ukweli. Siasa na kila kitu ndo maana mwalimu Nyerere alihimiza sana elimu ya siasa. Mtz wa sasa akiskia unaleta habari za siasa atakuona ni mtu mjanja mjanja mweny kutaka kumuibia. Hii hutokana na wanasiasa tulio nao...jamii inawachukulia kua ni wezi kwa hiyo mwananchi hataki kujihuaisha na siasa.

Udini na ukabila. Hili ndo tatzo kubwa hata suluhisho lake linakua gumu. Na ccm wanajitahid kutumia huu udhaifu kwagawa watz.
All-in-all hatupaswi kukata tamaa. Twahitaj kusimama imara, kuongeza juhudi endapo tu tutapata mtu wa kutuongoza kudai haki zetu zinazoendelea kiporwa na hawa mabeneru weusi wanatuitao wanyonge ilihali wanatung'ata na kututafuna bila huruma.
 
Swali zuri sana lakini mitazamo yako ya Kwa nini tunashindwa kuitoa CCM madarakani ndio chanzo cha kushindwa kuitoa CCM madarakani
Siri ya mtu kutatua matatizo yake ni kujua Kwa ukweli bila kujidanganya chanzo cha ukweli wa matatizo yake,hapo sasa ukiwa na dhamira ya dhati kabisa ya kutatua hayo matatizo utafanikiwa
 
Wengi wape. Kama mko wachache kura zenu hazitoshi.
 
Huko kote ulipotaja kuna nini wamekipata baada ya hayo Mapinduzi?

Libya wanachinjana kama Mbuzi Kule Vingunguti
Kule Egypt Al Sisi anapeleka mswaada Bungeni atawale Mpaka 2030 n.k
Hiyo ni transition period tu hata mataifa yaliyoendelea yalipitia huko huko, dawa kuwatoa kwanza madikteta alafu mipango baadae.Ukisema mjipange kupata taasisi imara ndani ya CCM ndio muitoe mtajipanga mpaka lini? Itakuwa ni ndoto, hizo nchi ulizozitaja zitakuja kusimama vizuri tu, hivi mtu kama Yahya jammeh ulitaka aendelee tu kuwepo madarakani kule Gambia? Inabidi ufike muda tuseme enough is enough.
 
Huo uoga utaishaje? Mbona wenzetu wanaweza sisi tuna nini tumelogwa au?
 
Mkuu kuanza kuhangaika kumtoa mbowe sasa hivi ni kuwapa points tu CCM, cha muhimu nani tumpe kura zetu 2020 Lissu, Zitto?
 
Write your reply...
kuna kitu ambacho watanzania wengi hawakijui.
Ni kwamba ukisha sema nchi ni ya kidemokrasia ina maana nchi iko mikononi mwa wananchi, wananchi ndio wamiliki wa nchi na ndio wenye maamuzi ya mwisho, wananchi ndio wamiliki wa ngazi zote za uongozi, kwasababu tunaposema wananchi tunamaanisha wote mradi awe mtanzania wa asili. wananchi ndio wanawajibu wa kuwachagua viongozi wenye sifa wanaowataka ili kuwaongoza wananchi hao katika kuendesha shughuli za kimaisha. kwahiyo wananchi ndio wenye mamlaka ya kumkubari mtu kua kiongozi au kumkataa sababu wenyewe ndio wenye uhitaji, sasa inapotokea wenye uhitaji mnamuhitaji john kwa sifa zake halafu anatokea mtu au kakundi fulani kanakuja na mtu wao, kwa manufaa yao kana mpakachika kwenye Kiti cha uongozi ambacho ni kihalisia ni mali ya wananchi bila ya ridhaa yao, halafu hao wananchi wanakaa kimya bila ya kuleta upinzani utakaoashilia kuokubariana na hicho kitendo ni kutoa mwanya wa kuendelea kukandamizwa milele. Wananchi watambue kua nafasi za uongozi ngazi zote kuanzia ngazi ya ubalozi wa nyumba kumi, vitongoji, vijiji/ mitaa, udiwani, ubunge na urais ni mali yao, wananchi ndio wenye mamlaka wa kuweka viongozi katika ngazi hizo kulingana na sifa wanazotaka na wala si vinginevyo, sasa mnapopachikiwa midubuwasha msiolitaka halafu mkakaa kimya maanake mumekubariana nalo waliopachika watakua hawana makosa, nyie si mumekubari bana.
 
Elimu ya Uraia Ndio itakayo itoa ccm madarakani, pale wananchi watakapo fahamu haki zao za msingi kuzipata kupitia kwa serikali. Kuwapa maji, umeme, Elimu, afya, miundo mbinu sio favor, ni wajibu kwa serikali kuwapa wananchi.

CCM wana wa fanya wananchi wajinga, kila wanalo fanya kupitia serikali ni favor na kwamba vyama vyengine vyenye agenda tofauti haviwezi kufanya, Elimu inahitajika na hizi Ngo Ndio chachu ya maendeleo, wazidi kutoa Elimu ya Uraia.

Naamini kama zitafanyika jitihada ndani ya miaka mitano kwa speed, wananchi watabadilika na ujinga wa kubeba bendera za siasa na t-shirt zitawekwa pembeni na utaifa kwanza utakuwa mbele ukiwa na haki za wananchi wote kwa ujumla.

One day.. Don't give
up
 
Mku kuna kitu nakiona ni hatari kwani Watu kama Lusu na wengine wengi wakiamua kujitoa kwenye vyama na kuja kiuanarakati na kupitia hii sheria mpya ya vyama.

Hii hakuna mtu anaweza kuwazuia hawa watu waliochoka kwani kuna mahali wamekosa mshika kibendera cha kuwaonyesha njia ya kupitia
 
Amani italindwa kwa gharama zote
Kama umeichoka sogea Burundi au Congo

Tanzania kipaumbele cha kwanza ni amani
CCM sio amani acha kupotosha, na tulipo sasa Tanzania amani hakuna tena tumebaki kuvumiliana tu.
Uvumilivu nao unatoka tutafika pale mnapo paogopa.
Endeleeni kua na kibri!
 
Tuachane na Siasa, Tuendelee kubet tuu, Maisha yasonge mbele ! Hakuna Namna.....
 
Katika nchi nyingi za Afrika Mashariki na Kati kinachoamua mshindi sio sanduku la kura.We tazama tu mifumo yao ya uchaguzi;ni hadaa tupu.Akili ya kawaida tu haikutumi kabisa kwenda kusimama mstari kupiga kura.
 
Nguvu na uweza vii mikononi mwetu watanzania. Kinachotukwamisha ni UOGA wenye chembe chembe nyingi za UJINGA.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…