Tangu wakati Mwalimu akiwepo kwenye madaraka au nje ya madaraka kulikuwa na changamoto kama taifa, na wale wanaotaka tuamini kwamba enzi za Mwalimu kulikuwa hakuna changamoto ni watu ambao hawataki kuukubali UKWELI. Lakini tofauti na viongozi wengine waliomfuata Mwalimu kwenye Urais, yeye alikuwa anazielezea changamoto zilizopo, anazichambua,anatafuta njia za kukabiliana nazo,anakabiliana nazo,anafanya tathimini kisha anatoa mwelekeo.
Enzi za Mwalimu kulikuwa na maandiko mengi sana yaliyoandikwa na yeye mwenyewe au yaliyotokana na maamuzi ya vikao kwa kufuata falsafa yake. Mwalimu aliandika vitabu, makala, vijarida na alitoa hotuba mbalimbali kuelezea mambo muhimu yahusuyo taifa. Kama mtu atachukua hatua ya kuyasoma au kusikiliza hotuba za mwalimu, basi bila shaka atagundua kwamba Mwalimu alijenga utaifa na kuusimamia utu wa watu wake.
Lakini tangu kuja kwa mfumo wa vyama vingi kumekuwa na kiwewe cha kushika madaraka na kuyang'ang'ania na kupoteza kabisa watu wanaojali nchi yetu inakwenda wapi. Kiuhalisia jamii nzima imetopea kwenye kiu kubwa sana ya "kupata" bila ya kujali huko kupata kunapatikanaje.
Sasa hivi hapa nchini kwetu kuna udini wa kutisha sana na kwa bahati mbaya Rais wetu Jakaya Kikwete aliishia kusema tu "...kampeni za uchaguzi mkuu zilitawaliwa na udini" bila ya kwenda kwa kina sana udini huo ulifanywa na nani dhidi ya nani. Matokeo yake kila mwananchi akatoka na Tafsiri yake.
Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba sasa hivi ni waislamu "moderate" peke yao ambao wanaweza kusimama hadharani na kusema wao ni CHADEMA damu damu. Na wakristo wengi hivi sasa hata waliomo ndani ya CCM wanaamini "waislamu" wana ajenda ya siri ya kuislimisha nchi na wanaitumia CCM kama chombo cha kufanikisha azima yao hiyo. Hali ya kutokuaminiana kati ya dini hizi mbili ni mbaya kiasi kwamba hata ukiona viongozi wa dini hizi wanachekeana hadharani unatia shaka kutokana ya yale yanayotokea na kupangwa sirini!!
Tanzania (siyo Tanganyika wala Zanzibar) ilijengwa wakati wa vuguvugu la umajumui wa kiafrika (Panafrikanisim). Tanzania hiyo ilikuwa Tanzania ya watu wote kwa maendeleo ya watu wote na kila mtanzania aliwaamini viongozi wake na wao waliamini katika dhana ya "serikali ni wananchi" na 'cheo ni dhamana" Kila jambo lilikuwa letu sote ingawa tofauti ilikuwepo.
Tanzania ya leo kama mwaka 1995 Mwalimu aliiona ina "nyufa" basi bila shaka hii ya sasa baadhi ya kuta zake zimeshaanguka na kila apitaye nje anaona kilichomo ndani. Hakuna tena anayeutaka Muungano (wapo wanaojidai kuutaka) na wala hakuna tena anayejali kama ukivunjika kitatokea nini.
Tanzania ya leo watu wanaamua kuwa wanachama (siyo wafuasi) wa chama fulani si kwa sababu za kupenda sera,Itikadi au falsafa ya chama husika, bali kwa sababu chama hicho kinamhakikishia uwezo wa kushinda uchaguzi ili apate "ulaji' au njia za kujinufaisha yeye mwenyewe.
Watu hawasomi tena kwa ajili ya kuongeza maarifa ili wakaitumikie jamii inayowahusu, bali siku hizi kusoma ni zana mojawapo inayomsaidia mtu kuongeza nafasi ya kupandishwa cheo au kuongezwa mshahara. Hali hiyo imesababisha watu kuvurugana na kukanyagana kwenye kughushi vyeti au hata kuhonga ili "wafaulu' mitihani kwa kiwango cha juu sana (GPA?) kwa lengo la kuonekana "wasomi" bila ya kujali kama wana elimu stahiki kwenye fani husika.
Maadili kwenye jamii yetu yameshapuuzwa siku nyingi sana. Mtu kuanzisha NGO ya kulelea watoto Yatima kwa lengo la kupata fedha za kuanzishia miradi yake binafsi si kosa la jinai tena. Ni sehemu ndogo sana (kama bado ipo) ambayo haijihusishi na ufisadi huu wa kimaadili. Wazazi, watoto na wanajamii wote tunaufurahia mmomonyoko huu wa maadili kwa sababu tu unatufaidisha kwa namna moja ama nyingine.
Mtazamo wangu kama jamii ya Tanzania tukiendelea namna hii basi bila shaka huko tuendako siku si nyingi taifa letu LITASAMBARATIKA!!
Ndiyo tatizo letu watanzania kujigeuza mbuni kutumbukiza kichwa shimoni wakati mwili woote uko nje. Mimi nina mahusianon na wakristo na waislamu ambao pia ni wanasiasa.Usingeweka aya hiyo yenye maandishi mekundu ungekuwa mfano wa kuigwa wa warushaji wa THREADS zenye mantiki na zinazojadilika. Maandishi mekundu yamedhihirisha kweli kuna udini na wewe ni mdini namba moja Kwa nini CCM na Uislamu? Kwa tafsirim hiyo una maana CHADEMA na UKRISTO?. Thread imekosa ladha tena, acha nijiondokee. Jamani tujadili masuala yahusuyo kuitenga Tanzania imara na siyo majungu haya.
Mkuu wangu umeandika yote lakini ulipofika hapo ndipo umechemsha vibaya sana. Kwanza hakuna kitu - Muislaam moderate hii habari umeipata wapi?..Lakini ukweli ulio wazi ni kwamba sasa hivi ni waislamu "moderate" peke yao ambao wanaweza kusimama hadharani na kusema wao ni CHADEMA damu damu. Na wakristo wengi hivi sasa hata waliomo ndani ya CCM wanaamini "waislamu" wana ajenda ya siri ya kuislimisha nchi na wanaitumia CCM kama chombo cha kufanikisha azima yao hiyo. Hali ya kutokuaminiana kati ya dini hizi mbili ni mbaya kiasi kwamba hata ukiona viongozi wa dini hizi wanachekeana hadharani unatia shaka kutokana ya yale yanayotokea na kupangwa sirini!!
Mkuu wangu umeandika yote lakini ulipofika hapo ndipo umechemsha vibaya sana. Kwanza hakuna kitu - Muislaam moderate hii habari umeipata wapi?..
Na kwa nini watu mnapenda sana kuutafsiri Uislaam wakati nyie sio Waislaam? na wala hamjui lolote kuhusu Uislaam!. Kuwepo kwa Waislaam CHADEMA ni kwa sababu hatupendi UDINI japokuwa upo na tunatazama Chadema kama chama cha siasa na sio jumuiko la watu, Chadema kama mbadala na sio kuwepo kwa Dr.Slaa au Mbowe na dini au kabila lake. Hivyo tayari wewe mwenyewe inakuweka ktk UDINI unapojaribu kujenga hoja kwa kutumia dini za watu na hata kuwa label waislaam kama moderate...
Marekani pia wanapenda sana kutumia neno hilo, lakini ukweli utabakia kwamba wale waislaam wanaopingana na Marekani ni kwa sababu Marekani inafanya Ugaidi (terrorist) nchini mwao kuwaibia mafuta na rasilimali zao kwa kuwaweka vibaraka wao. Sasa kwutokana na kwamba nchin hizo asilimia 99 ni waislaam basi mpiganaji yeyote ataitwa Muislaam mwenye siasa kali na sio Mu -Afghanstan, Iran au Iraq. Ukweli utabakia kwamba hao wangekuwa Wakristu wangelifanya hivyo hivyo maadam ni Marekani iliyowaingilia tawala za nchi zao lakini hakuna kosa kabisa wao kujitambulisha kama nchi ya kikristu- na hata wanajeshi wao hsusali kikristu kabla ya kwenda vitani nchi za watu lakini wao hawapewi jina wala kuitwa wakristu isipokuwa Marekani au NATO. Msitake kabisa kuchanganya Uzalendo wa wananchi kwa sababu tu ni Waislaam..
Tanzania Udini upo na unatokana na kwamba Wakristu wanajiona wao wabora zaidi ya Waislaam nan pale waislaam wanapopinga mfumo uliopo mnawaona wao ndio wadini japokuwa ukweli hamtaki kuutazama. Na kama Chadema wanafikiria hakuna tatizo ama waislaam ndio wakorofi basi mnatuweka hata sisi tunaofikiria tunaweza kuyapata mageuzi kupitia Chadema kutokuwa na imani na chama hicho...
Mkuu wangu na wewe nisome vizuri. Nazungumzia kitu kinachonihusu mimi na Waislaam. Ulichoandika hapo juu ni mawazo yako ukisisitiza ni ukweli uliopo wazi ya kwamba waislaam moderate ndio wapo Chadema..I am not a moderate Muslim na hakuna kitu hicho. Ufunge na ufungue haipotezi maana kwamba haya ni maneno yako kwa fikra zako kama ulivyoandika hapo juu. Nimeingia Chadema kwa sababu naipiga vita CCM na mfumo wake wa kiutawala haijalishi ndani ya CCM au Chadema kuna watu gani ama ndio U moderate. Hao wanaofikiria Uislaam na Ukistu ndio wanapenda sana kutugawa ktk makundi haya na wapo wajinga wanaamini hivyo kuendeleza kutuita sisi moderate ni kutuwekea mzigo tusio ubeba..Mkandara tatizo ni wewe kwa sababu hata hapo nimeandika kuna baadhi ya "wakristo" ndani ya CCM wanahisi kwamba hawatendewi haki kwenye uteuzi wa nafasi mbalimbali. Mkandara mimi na wewe tumo kwenye tatizo ninaloliongela na ndiyo maana kwenye bandiko zima unadai nimechemsha kwenye kusema kuna waislam "moderate". kwani kule shuleni tulifundishwa kwamba mtu akiweka alama hii ya funga na fungua usemi anamaanisha nini? Maana yake icho alichoandika hakiko hivyo kilivyoandika au hakuna hakika ya hicho kilichoandikwa.
Huwezi kuniambia kwamba kina Basalahe na wenzake na Redio Imaan ya Morogoro msimamo wao dhidi ya CHADEMA umejengwa kwenye misingi ya tofauti ya sera za CHADEMA kisiasa. Halafu hata mimi najua kuna wachungaji na vingozi wengine wa kanisa wanaiunga mkono CHADEMA si kwa sababu wamefurahishwa na sera zake bali ni kwa sababu ni chama "chao" kwenye muktadha wa siasa za Tanzania.
Soma vizuri bandiko langu utagundua kwamba mimi ninachosimamia si huu "uislam' au "ukristo" unaosimama kwa misingi ya kisiasa. Mimi nawajua waislam na ninaheshimu sana waislam kwani ni ndugu zangu kama walivyo wakristo ambao pia ni ndugu zangu. Msiugeuze huu mjadala kuwa wa kidini.
Mkandara said:Tanzania Udini upo na unatokana na kwamba Wakristu wanajiona wao wabora zaidi ya Waislaam na pale waislaam wanapopinga mfumo uliopo mnawaona wao ndio wadini japokuwa ukweli hamtaki kuutazama.
Hivi mkandara unataka kuniambia kwamba ni rahisi kwa Muislam kusimama Mtambani au kwa Mtoro na kusema kwamba yeye ni mwana CHADEMA kindakindaki na wenzake wakamuelewa!! Hivi unataka kusema leo hii hujui kwamba kuna Wakristo lukuki wanaiunga mkono CHADEMA kwa sababu ni chama "chao?" Baada ya uchaguzi wa Uzini si tuliambiwa kwamba CHADEMA ilikuwa ya Pili kwa sababu eneo hilo lina wakristo wengi huko Zanzibar. Hii maana yake ilikuwa nini Mkandara? Mimi situngi hadithi bali naongea kile kilichopo hata kama kitu hicho sikiamini!!Mkuu wangu na wewe nisome vizuri. Nazungumzia kitu kinachonihusu. Ulicvhoandika hapo juu ni mawazo yako ukisisitiza ukweli ulkio wazi ya kwamba waislaam moderate ndio wapo Chadema..I am not a moderate Muslim na hakuna kitu hicho. Ufunge na ufungue haipotezi maana kwamba haya ni maneno yako kwa fikra zako. Niomeingia Chadema kwa sababu naipiga vita CCM na mfumo wake wa kiutawala haijalishi ndani ya Chadema kuna watu gani. Hao wanaofikiria Uislaam na Ukistu ndio wanapenda sana kutugawa ktk makundi haya na wapo wajinga wanaamini.
Na siwezi kuwatetea wakristu kwa sababu sijui wanajiunga na CCM au Chadema kwa ajili gani isipokuwa kile wanachokizungumza au kutetea. Naweza tu kuwakosoa kwa yale wanayoyaandika au kuyasema lakini siwezi kusema kwamba wakristu waliopo Chadema ni wale wanaopingana na Uislaam kwa sababu sijui fikra zao wala hisia zao ila wao wenyewe. Sote tunaheshimiana lakini sio la kubandikiana kwa nini tupo Chadema kwa sababu sio kweli hata kidogo.
Hakuna muislaam anayeweza kusimama msikiti wa Mtoro na akasema yeye ni CCM wala CUF isipokuwa atazungumzia adha na machafu yanayofanya dhidi ya wananchi au dini yenyewe. Kwa hao mnaowaita waislaam wanaposimama majukwaani na lkulalamika ni muhimu zaidi kuwasilikiza na kuutazama ukweli na sio dini zetu kwa sababu lisemwalo lipo!..Hivi mkandara unataka kuniambia kwamba ni rahisi kwa Muislam kusimama Mtambani au kwa Mtoro na kusema kwamba yeye ni mwana CHADEMA kindakindaki na wenzake wakamuelewa!! Hivi unataka kusema leo hii hujui kwamba kuna Wakristo lukuki wanaiunga mkono CHADEMA kwa sababu ni chama "chao?" Baada ya uchaguzi wa Uzini si tuliambiwa kwamba CHADEMA ilikuwa ya Pili kwa sababu eneo hilo lina wakristo wengi huko Zanzibar. Hii maana yake ilikuwa nini Mkandara? Mimi situngi hadithi bali naongea kile kilichopo hata kama kitu hicho sikiamini!!