Tunaibiwa!

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Baada ya kusoma post nyingi na kufuatilia kasumba la Umeme Tanzania, Hitimisho limekuwa simple: CCM IMETUPIGA CHANGA LA MACHO. Lakini cha kufurahisha zaidi ni kwamba hii haikuwa mara ya kwanza. Ni bao lililopo kwenye ligi moja na la EPA na Richmond. Ninachojiuliza kwa sasa bao la 2015 litakuwa nini?

Kwanza walianza kwa kutuzungusha-zungusha na vikao vya Halmashauri Kuu ya Chama iliyomswali Spika, mara sijui TRL na hao wahindi. Lakini kumbe zote hizi zilikuwa njama za kutuvuruga akili, kwa kusudi tusishtukie bao lililofuata! Bao lenyewe ni IPTL kulipwa Tsh23 Billion a month. Ivi watu wangapi wanajua hao IPTL ni nani? Ivi hii pesa tunaijua au ni kuitamka tu? Wabunge wetu wamelala au vipi? Nadhani wananchi wangependa kuona na kusikia kelele zaidi kutoka bungeni, pamoja na mahesabu ya hayo malipo tulipayo kila kukicha.
Jamani bei ya Magenerator mapya ya umeme ni kiasi gani? Bei ya kuyasafirisha mpaka hapa ni kiasi gani? Mbona tumefanywa kama Makondoo yasiyojua kitu? Mbona nchi yetu inageuzwa kuwa Pango la Wanyang'anyi?
Mpambano wa kuiondoa CCM ni sawa na ule uliomuondoa Mkoloni. Na ukweli ndo huu...CCM ndio chanzo cha matatizo yetu. Tunahitaji ukombozi mpya. I say: No More to CCM. Ningeomba kila mtu atakaye post hapa amalize kwa hii sahihi: NO MORE CCM.



Zifuatazo ni threads zinazozungumzia hili CHANGA LA MACHO:
1. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ikuwa-sahihi-na-kamati-ya-bunge-ilikosea.html
2. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/41106-siri-yafichuka-umeme-tatizo-sugu.html
3. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/41056-power-crisis-tough-times-ahead.html
4. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...aifishwe-serikali-yapinga-mgao-waendelea.html
5. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...aamuru-mitambo-ya-iptl-iwashwe-mara-moja.html
6. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/41888-can-iptl-save-us.html
7. https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-juu-zaidi-ya-mara-6-kulingana-na-dowans.html
8. https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/10842-ufisadi-the-making-of-iptl.html
 
mi nadhani ungeakikisha kwanza hizi habari kabla atuja itikia no more ... lakini kutoa accusation purely based on previous posts ambazo zimo JF tutajikuta tunalipoka na kuitwa Miafrica.
 
Hakuna cha kuibiwa sisi ndo tulivyo.Nafikiri umeangalia kwa mtazamo mwepesi zaidi.
 
mkuu umepiga kura serikali za mitaa?
nina hakika wahusika wangu wamepiga. Mimi binafsi siwezi kupiga
mi nadhani ungeakikisha kwanza hizi habari kabla atuja itikia no more ... lakini kutoa accusation purely based on previous posts ambazo zimo JF tutajikuta tunalipoka na kuitwa Miafrica.
soma hizo reference nilizoweka hapo...then come to ur own conclusion! Sijakunyima kuja na conclusion yako mh. Na kama unaona ni uongo...tungependa maelezo zaidi
Hakuna cha kuibiwa sisi ndo tulivyo.Nafikiri umeangalia kwa mtazamo mwepesi zaidi.
Una maana gani kwa kauli ya "sisi ndo tulivyo"? Mtazamo mwepesi ndo upi?
 
nina hakika wahusika wangu wamepiga. Mimi binafsi siwezi kupiga

soma hizo reference nilizoweka hapo...then come to ur own conclusion! Sijakunyima kuja na conclusion yako mh. Na kama unaona ni uongo...tungependa maelezo zaidi

Una maana gani kwa kauli ya "sisi ndo tulivyo"? Mtazamo mwepesi ndo upi?

Tuna tatizo la sisi ndo tulivyo.Tafakari ama piga picha ya hisia kutokana na experience uliyonayo ya maisha yetu.
ndugu/jamaa akipatwa na shida ni nini aproach yake/yetu ya kwanza kabisa ktk ku solve tatizo??
 
Tuna tatizo la sisi ndo tulivyo.Tafakari ama piga picha ya hisia kutokana na experience uliyonayo ya maisha yetu.
ndugu/jamaa akipatwa na shida ni nini aproach yake/yetu ya kwanza kabisa ktk ku solve tatizo??

Sina uhakika na jibu la swali lako. Lakini kwa mawazo yangu mara nyingi hatujisumbui nao. Kwanza tunasherekea shida za wenzetu. Alafu pili watu hawajashtukia hili kabisa. Kama wameshtuki, basi wamejua wamepigwa BAO la nguvu. Pesa za Uchaguzi 2010 ndo hizo tena.

i say NO MORE CCM
Imefika muda wa kujiokoa kutoka nira ya CCM
 
Dawa yao ipo jikoni. Ngoja tutoshe 2015 tunawaondoa wote hao. watanyooka tu. Tanzania Bila C.C.M inawezekana bwana
 
Bao lenyewe ni IPTL kulipwa Tsh23 Billion a month. Ivi watu wangapi wanajua hao IPTL ni nani?

mimi niliwahi kusikia tu[kwahiyo ni tetesi tu hizi]kwamba
-wakati mchakato wa kuileta/kuitengeneza IPTL muungwana alikuwa pale wizara ya nishati na madini
-kwamba baada ya IPTL kuja/kutengenezwa muungwana alihamishiwa wizara ya fedha ambako alimbadili waziri aliyekuwepo pale ambaye inasemekana hakuwa ameikaribisha IPTL,na alitakiwa mtu pale wizara ya fedha ambaye hana tatizo na ujio wa IPTL kwasababu wizara hiyo ina role yake linapokuja suala la mikataba ya namna hiyo.
-kwamba muungwana akiwa pale fedha[kama alipokuwa kule madini]aliidhinisha kadili ka IPTL kupata tusenti twa kuazia mradi
-na tetesi hiyo niliyoisikia enzi hizo inamalizia kwamba huo ndio ulikuwa mwanzo wa uswahiba wa muungwana na mzee ruksa hadi akafikia kumbeba kwenye vikao vya chama hasa kuundoa ile kipengele ya mjumbe mmoja kupiga kura tatu,

kwahiyo mkuu hiyo ndio tetesi niliyosikia kuhusu swali lako,kama halijakidhi[kitu ambacho kinawezekana]wakuu wengine wataleta data hapa
 
Back
Top Bottom