Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,675
Baada ya kufunga ndoa Abdul alihama nyumbani kwao, alitafuta chumba mtaa wa pili dakika tano tu kutoka nyumbani kwao. Hii ilimfanya kuwa karibu na familia yake, mara kwa mara akitoka kazini alipenda kwenda, kupiga story na hata kula chakula cha usiku kabla ya kurejea kwa mkewe.
Mama yake alimvumilia kwa mwezi mzima akidhani tabia hiyo itakoma lakini haikukoma siku moja akaamua kumtolea uvivu alimuuliza. “Hivi ni muda gani unakaa na mkeo? Maana muda wote uko kazini na ukitoka kazini uko hapa? Huyo mkeo hana wivu?”
Huku akijichekesha chekesha “Mama na wewe, inamaana ushanichoka mwanao…” Mama Abdul hakujibu alimkodolea macho akitaka jibu. “Mke wangu hana wivu, yule mzungu Mama, kwanza anajua niko hapa hivyo hata nikienda nimeshiba hajali…”
Kabla ya kumaliza Mama yake alimpiga makofi mawili ya nguvu. “Pumbavu! Mtu umezaliwa Marangu unajifanya mzungu! Ungejua mke wako anavyoumia usingejichekesha chekesha hapa na Dada zako! Umehsaoa nenda ukakae utulie na mkeo sio kujifanya unatupenda sana!
Sitaki kukuona hapa! Ukikanyaga tena kwangu labda nimelazwa hospitali! Vinginevyo nijulie hali kwenye simu basi! Nanyie mbuzi (Akiwageukia watoto wengine) kaka yenu ameshaoa, mpeni pumzi na mkewe! Muacheni binti wa watu afurahie ndoa yake, sio kujipeleka peleka kila siku!
Siku nikisikia mmeenda enda tu na kwangu msirudi! Mwanangu hawa dada zako watakuvunjia ndoa yako, mkeo anavumilia tu lakini anaumia, hakuna mwanamke anapenda kupika chakula halafu kikapoa, akahangaika kukipasha halafu unarudi unamuambia umeshiba! Nimekula kwa Mama! Kama ulikuwa bado hujamalizana na Mama yako kwanini ulioa?”
Alimaliza kuongea, nyumba yote ilibaki kimya. Mama Abdul alikuwa mpole lakini akikasirika wote hukaa kimya. Watoto walimgeukia Baba yao na kumuangalia kama atasema kitu. “Mnaniangalia nini? Fuateni maelekezo ya Mama yenu, mimi mwenyewe aliniambia hivyo hivyo miaka 30 iliyopita na mpaka sasa tuko pamoja”
Kimya kimya Abdul alinyanyuka na kuanza kuondoka lakini kabla hajfika mbali Mama yake alimuambai “Halafu mwezi ujao unahama, sitaki kukuona mtaa huu wala mtaa wa jirani, kwakifupi sitaki kukuona kabisa Temeke, hamia huko Mwenge au hata Sinza, sitaki kukuona karibu. Katulie na ndoa yako, sitaki kuja kuja kwako bila sababu..” Alimaliza, huku akimsindikiza akamtoa nnje na kufunga mlango.
HUU PIA NI UPENDO WA MAMA KWA KIJANA WAKE....