Tunahitaji tume ili kujua Mawaziri wengi wa Muungwana...

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,029
kazi imewashinda wamekalia kuboronga tu!? Haya mamilioni kama sio mabilioni yaliyotumiwa na tume hiyo yangeweza kuelekezwa kwingine ambako yangeleta manufaa makubwa. Usanii kama kazi!
Posted Date::1/13/2008
Tume ya Mkandara yawachanganya mawaziri
*Ni ile inayochunguza utendaji wao wa kazi

*Wasema inawakatisha tamaa katika kazi zao


Na Waandishi Wetu
Mwananchi

TUME iliyoundwa kwa siri na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza utendaji wa mawaziri wa wizara mbalimbali tangu awachague hadi sasa imewachanganya baadhi ya mawaziri kwa kushindwa kufahamu nini hatima ya nyadhifa zao.

Baadhi ya mawaziri sambamba na manaibu wao, ambao baadhi walionyesha kuchukizwa na hatua hiyo ya kuwekewa watu wa kuwatathmini, huku wakifafanua kuwa kitendo hicho kinawadhalilisha na kuwakatisha tamaa katika uwajibikaji wao.

"Unajua unapowekewa watu wa kukuchunguza bila kuwa na taarifa na kisha ukawabaini unakuwa na walakini na mwajiri wako. Sisi tunatazama lolote linaloweza kutokea maana uwaziri tuliukuta na tutauacha," waziri mmoja aliliambia gazeti hili.

Taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali serikalini zinaeleza kuwa, tume hiyo ilipewa siku 60 kukamilisha kazi hiyo na sasa ripoti inaandikwa kabla ya kukabidhiwa kwa rais.

Hivi karibuni gazeti moja la kila wiki lilichapisha habari kwamba ripoti hiyo imekamilika, lakini chanzo chetu kimesema bado kazi ya kuunganisha taarifa inaendelea na inaweza kukamilika katikati ya Februari.

"Si kweli kwamba ripoti imekamilika kama ilivyoelezwa huko nyuma. Tunachokifahamu sisi ni kwamba tume inaunganisha ripoti, maana ilipewa siku 60 kuanzia mwezi Desemba 2007," chanzo kimoja kilisema na kuongeza;

"Nakumbuka kazi hii ilianza katikati ya Desemba na kama nitakuwa sijakosea basi itakamilika katikati ya Februari 2008."

Kwa mujibu wa chanzo kingine; tume hiyo inayoongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, imemaliza kazi ya kupitia taarifa na uchunguzi katika wizara mbalimbali hadi sasa na kazi iliyopo mezani ni kuunganisha taarifa kisha kuzifikisha kwa Kikwete.

"Rais aliunda tume hiyo kwa siri, lakini si unajua nchi hii ilivyo sasa? Mambo yote yako wazi na sasa inafahamika. Sijui kama itaweza kufanikisha lengo maana wakubwa wanatazamana na wanaweza kuwafahamu wanaowachongea kama wakienguliwa," chanzo hicho kilidokeza.

Inaelezwa pia kuwa, usiri wa tume hiyo inayojumuisha vigogo wa juu katika Redet ulianza kupotea baada ya wajumbe hao kuanza kufanya ziara katika wizara mbalimbali na huko walikuwa wakiwahoji mawaziri na makatibu wa wizara hizo.

"Ninachofahamu kwa kweli kazi inaendelea, lakini ni kwa siri mno. Kazi hii inafanywa na vigogo wa Redet ni vigumu kubaini nini kilichomo, lakini siku zinavyokwenda tutapata ukweli," chanzo chetu kingine kutoka UDSM kilieleza.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, tume hiyo iliundwa baada ya utafiti wa awali wa Redet kubainisha umaarufu wa Kikwete kuwa juu ya ule wa Baraza lake la Mawaziri.

"Rais aliamua kuufanyia kazi utafiti ule na ndio maana akaunda tume hii. Lengo ni kutazama na kupata taarifa za kitaaluma kuhusu baraza hilo na kama linakidhi haja iliyopo kwa wakati huu," chanzo chetu kilifafanua.

Profesa Mukandara alipoulizwa kuhusu suala la yeye kuongoza tume hiyo, hakukataa wala kukubali huku akisema; "aah sasa hayo...niulize siku, alisema.

Baadhi ya vigezo vinavyotumiwa na tume hiyo katika kuchunguza ni pamoja na namna waziri anavyoonekana katika jamii, uwezo wake wa kutenda kazi, mafanikio aliyofikia tangu achaguliwe, nidhamu ya kazi na namna anavyoweza kumudu sifa za utawala bora.

Mwanzoni mwa Desemba mwaka jana, Redet ilitoa ripoti yake ya utafiti juu ya utendaji wa serikali na kubainisha kuwa utendaji wa mawaziri ulikuwa umeshuka, jambo ambalo wachunguzi wa mambo walisema mawaziri hao ni mzigo kwa rais na kumshauri afanye mabadiliko.
 
kazi imewashinda wamekalia kuboronga tu!? Haya mamilioni kama sio mabilioni yaliyotumiwa na tume hiyo yangeweza kuelekezwa kwingine ambako yangeleta manufaa makubwa. Usanii kama kazi!
Bubu, huwa nina kawaida ya kuwahi kwenye kivuko saa 7 mchana ili kumdaka yeyote aliyetoka Mwanza na gazeti. Leo nimekumbana na jamaa ana Mwananchi, nilipoona Tume ya $IRI nikashika kichwa huku miguu ikipoteza nguvu!!

Yego nimejiuliza mambo mengi sana:
1. hivi, inawezekana kusafisha uoza unaotoa harufu ndani ya nyumba yako ikahitaji msaada wa jirani? Mbona hapo nyuma hii ilikuwa aibu ya kuimaliza ndani kwa ndani?

2. ...na utakapoambiwa kuna uchafu unanuka ndio uusafishe? Yaani pua zako mpaka uazime za jirani? Au kusafisha ndio kumekushinda?

3. ...vp kama jirani akisema harufu sio kali, utaendelea kukaa ndani ukiwa umeziba pua kisha kupumua kwa mdomo kwa sababu wenyewe haunusi!

4. ...utakapoendelea kupumua kwa mdomo kisha harufu ikawakera wanaokuzunguka na kuamua kukutoa humo kwenye nyumba (2010), kweli utalalamika? Au ndio unapumua kwa mdomo huku ukijiandaa kufanya mchezo mchafu kabla hawajakutoa?

5. ...vile vile, huna wasiwasi kwamba kuendelea kupumua kwa mdomo kunaweza kusababisha matatizo mengine hata kabla ya wanaokuzunguka kukutoa (2010)? Matatizo kama kansa ya koromero!!

Yego, yaani hii ni aibu. Lakini pia haka ni kamchezo ka kutengenezeana visenti ili huyu jamaa wa Choo Kikuu, ambaye pua zake zinanusa sana, atunishe mfuko maana alizikosa zile BoT na wala hakupata hisa kwenye maBuzwagi. Aaah, hawawezi kumtupa yego, jamaa amekuwa mdau tangu mwaka 1995 kuhalalisha ushindi.
 
huyu muungwana anatuboa na matume yake kibao.

kila kitu tume, na hizi tume zinanyima maendeleo maana mijihela yote tunamaliza kwenye tume.

mambo si yako wazi na kama mfanyaji afanye tu asitutie nyege za kijinga
 
Back
Top Bottom