Tunahitaji muuzaji wa duka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji muuzaji wa duka

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mipango, Oct 16, 2011.

 1. m

  mipango Member

  #1
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tunahitaji msichana kwa ajiri ya kazi ya kuuza bidhaa mbalimbali ktk duka letu.

  Majukumu ya kazi husika ni kama ifuatavyo:-

  1. Kukaribisha na kuhudumia wateja kwa ujumla
  2. Kupanga bidhaa kwenye ngazi
  3. Kuandika order za wateja
  4. Kupokea simu za wateja
  5. Kuandaa ripoti fupi ya mauzo ya kila siku nk.

  Sifa za muombaji.
  1. Awe mwaminifu.
  2. Awe mchangamfu.
  3. Awe mchapakazi.
  4. Awe mwenye nidhamu
  5. Awe anaishi Dar es salaam
  6. Awe na kiwango cha elimu kuanzia kidato cha nne hadi kidato cha sita
  7. Awe na uzoefu wa biashara au awe amepitia mafunzo ya biashara
  8. Awe na umri kuanzia miaka 18 mpaka 30.


  Maombi yote yatumwe kwa njia ya e-mail hii;
  mipango2011@yahoo.com

  Au unaweza kunipigia simu kwa maelekezo zaidi. Piga no.0779321400
   
 2. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mkuu. umenikumbusha wimbo wa bongo F, usemao "kazi yangu ya dukani ohh oh oh yaniweka matataniii eh eh....
  Lakini anyway ni fursa nzuri kwa anayehitaji kazi husika, basi akina dada changamkieni tenda.

  Ila kazi ya kuuza duka inahitaji uaminifu sana maana ukiwa mkono mrefu huchelewi kupigwa chini.Na tatizo kwa wabongo wengi neno uaminifu ni msamiati mgumu, pia kauli nzuri kwa wateja ni tatizo sana kwetu wabongo, eti unakuta muuza duka anasoma gazeti tena la udaku wala hata karibu hakupi, tena nyie akina Dada ndo mmezidi mapozi sana.

  ​
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mshahara sh ngapi?
   
 4. A

  Asuu Member

  #4
  Oct 16, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa mku mi nne mdogoangu.ila duka hilo likoapi? Au lipo maeneogani, yaani kwa ajiliya usafiri.
   
 5. m

  mipango Member

  #5
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu. mshahara ni maelewano baina ya mwajiriwa na mwajiri, ila tunazingatia viwango vilivyowekwa na Serikari pia.

  Asante
   
 6. m

  mipango Member

  #6
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu. tupo kariakoo. mtaa wa aggrey.
  Asante
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Tatizo mpaka watoto wa kike kwani watoto wa kiume hatuwez, hebu mkuu tupatie ajira vijana wenye jinsia tofaut au sio wadau? Maana mi ni mmoja wa wataftaj kazi ni hayo tu naomba uunde kamati ufikirie ombi langu!
   
 8. m

  mipango Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu.inkoskaz, ofisini kwetu tayari tumeajiri vijana wa kiume wengi tu, sasa tunataka kuleta uwiano wa kijinsia kwa kuajiri wasicha.

  Asante.
   
 9. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mimi niko tayari, au umeshapata mtu? Weka mshahara hapa kazi hizo ulizoweka hapo kila mtu anaweza kufanya labda kama ni mvivu kutoka tumboni mwa mamake.
   
 10. n

  ndaa New Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mkenya na niko tayari kwa hiyo kazi,tafadhali nipe nafasi.
   
Loading...