JEKI
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 4,845
- 2,966
Amini usiamini watanzania wengi hatupendi kufanya kazi.
Majuzi nilianzisha mradi na vijana wasiokuwa na kazi, ili tuunde kikundi cha kufanya kazi pamoja, nilichowaeleza vijana wale kikundi kile kitaongozwa na kauli mbiu ya mchango wako wa hali ndo muhimu kuliko mali.
Nikatoa ufadhiri wa kusimamisha project ndogondogo, nikawaambia vijana wale tufanye kazi hata za kuuza maji ya ndoa maeneo ya stand, tuuze hata juice ya makopo, icecream na hata tuwe na genge la kuuza chakula, amini usiamini vijana wale wamenikimbia, kila siku wapo kijiweni asubuhi hadi jioni hawana cha kufanya.
Hapo ndo nikaamini maneno ya viongozi wetu waliowahi kusema watanzania ni wavivu kufanya kazi.
Kwa hali niliyoiona tunahitaji muujiza tu kututoa hapa, hebu angalieni hata hapa JF, jukwaa hili ndo lina wachangiaji wengi, akiri zetu tumezielekeza kwenye mapenzi, vijana wale kila kukicha wanafukuzana na wanawake tu, kuvuta sigara na mengine ya ovyo.