Tunahitaji "FCC" katika elimu

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Haiwezekani mtoto huyu anasoma mambo A na mtoto mwingine anasoma mambo B, alafu mwisho wa siku tunawapa wote mtihani mmoja na kusema huyu kawa wa kwanza na huyu wa mwisho.

Kwanini tusiwe na comprehensive material moja ambayo kila mtoto ana access nayo na mitihani yote inatoka humo.

Haiwezekani tunakuwa na watoto wanakuwa over feeded, wanapewa kila kitu na kuna wengine hata basic materials kuzipata ni shida.

Ukichukua vitabu vinavyoelekezwa na wizara watoto kutumia, chukua na maswali ya mitihani, ni vitu viwili tofauti. majibu kwenye vitabu hamna.

Lakini kuna walimu wanafundisha materials nje ya silabusi na mambo hayo wanayofundisha ndiyo yamejaa kwenye mitihani na haya mambo yanasimamiwa na watu wanaojiita maprofesa.

Tunaposema elimu ya primary, secondary ni basic education, maana yake tunataka yale yote yaliyoko kwenye mitaala ya huko kila mtoto ayasome na kuyajua.

Ni jukumu letu kuhakikisha kila mtoto anapata kila taarifa na juhudi zake za kusoma pamoja na mda alioutenga kusoma pamoja na uwezo wake kuweka kumbukumbu viwe ndizo factor pekee zinazotuonyesha huyu ni bingwa na huyu hapana.

kwa mfumo wetu wa wengine kuwaficha taarifa na wengine kuwapa kila kitu tunaweza kuwa tunapata mabingwa "fake". Mabingwa halisi ambao wangefanya maajabu tunawatoe ulingoni kwa kuwanyima taarifa sahihi
 
Binti yangu alikuwa analala saa 6 usiku na 'kuamshwa' saa 10 alfajiri ili asome ………….., ki msingi binti yangu 'ali karirishwa' zaidi ya mwanafunzi wa shule ya kata anaye ingia darasani saa 2 na kutoka saa 7.30 mchana! Hata kama watapata same 'division', apo kuna mmoja ameumizwa, na hiki ndiyo tuna ipigia kelele wizara ya elimu kuhakikisha usawa unakuepo………..
 
  • Thanks
Reactions: ego
Back
Top Bottom