Tunahitaji Electoral Votes kwa Tanzania

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,842
Zina faida sana hizi Electoral Votes, Kwa Tanzania kila Mkoa utapewa idadi yake ya wajumbe (Utaratibu wa kuwapata wajumbe na sifa zao utawekwa kwa mujibu wa Sheria na kwa maridhiano ya wadau wote, Wajumbe hawa ni lazima wawe watu weledi, wasomi, wazalendo na watu Intelligent) Idadi ya wajumbe kwa kila mkoa itategemeana na wingi wa watu kwa kila Mkoa, Kwa mfano, kwa mkoa wa Dar. ambao una idadi kubwa ya watu takribani Zaidi ya milioni 4 utapewa idadi kubwa ya wajumbe, Faida ya kuwa na wajumbe hawa ni kwamba, Watanzania wengi hawajasoma au hawana akili timamu au hawana wanachokijua juu ya Nchi yao kwenye mambo ya UTAWALA, SIASA, UCHUMI nk.

Kwa mfano, Thamani ya kura ya mtu mmoja mmoja inatofautiana sana, kwa mfano, Kura ya msomi kwa mfano, wanafunzi wa vyuo vikuu au watumishi wa Umma au binafsi, profesa au Dr. ni tofauti sana na kura ya mtu ambaye si msomi wala si mtumishi.

Kwa mfano, Ukisema Prof. Kitila apige kura kumchagua X AU Y na ukasema mtu kama Lusinde apige kura hiyo hiyo kumchagua kati ya X AU Y ni vitu viwili tofauti kabisa, hivyo kunahitajika tuwe na Electoral Votes ziwe zinaamua nani Rais baada ya kupiga Popular votes.

Yawezekana matatizo ya watanzania yanasababishwa na kura za wapenda Rushwa wakati wa uchaguzi, watu wasio jielewa, watu waliokata tamaa ya maisha, au Uchama-Uchama, hivyo kuhitaji kura za ziada na muhimu kuamua nani Rais.
 
Ni kiongozi gani ndani ya ccm wa kukubaliana na hilo?sisi watanzania tukubali tu kwamba shetani ameshatu win hatuna jinsi,watu wa kwanza kukupinga kabla ya ccm ni viongozi wote wa dini..(unafiki umeshatuua)
Mi napita tu sina ugomvi na mtu.

"Not my president".
 
Sizani kama inawezekana Kwa Tanzania......

Kama inaweza kununua polisi na Tume ...

Ccm inaweza wanunua wote ....
 
Mi nafikiri tusiende kote huko kwenye Electoral votes.
Tuidai kwa nguvu zote Katiba mpya iliyotokana na rasimu ya Warioba ambayo itazaa Tume HURU ya Uchaguzi... Na sio hii takataka ya Lubuva.
 
Sizani kama inawezekana Kwa Tanzania......

Kama inaweza kununua polisi na Tume ...

Ccm inaweza wanunua wote ....


Ni kweli kwa Tanzania tunahitaji tujitoe haswa ili hili lifanikiwe, ila kwa kizazi hiki si rahisi, ni mjadala ambao tunaweza kuuanza taratibu
 
Mi nafikiri tusiende kote huko kwenye Electoral votes.
Tuidai kwa nguvu zote Katiba mpya iliyotokana na rasimu ya Warioba ambayo itazaa Tume HURU ya Uchaguzi... Na sio hii takataka ya Lubuva.

Mkuu hata ile Katiba ya Warioba uliona namna wajumbe wa Tume wanavyopatikana? acha kabisa, eti spika wa bunge, jaji mkuu nk. ndio watahusika na kuwapata hawa wajumbe wa Tume...!!
 
Electoral votes zinawaletea mtafaruku wamarekani. dawa ni kuwa kuwa na katiba mpya itakayojali sauti ya wengi.
 
Utaratibu wa uchaguzi wa marekani ni wa kishetani.Hauchukulii binadamu wote ni sawa.

Mfano mikoa tajiri ya marekani hupewa uzito mkubwa kuliko mikoa maskini kwenye kura.

wanagawa hivi

DAR ES SALAAM-MKOA UNAPEWA KURA 200
Kigoma unapewa kura 10
LINDI kura 5
Rukwa kura 5
dodoma kura 20
pwani-25
Zanzibar kura 30

Kwa hiyo ukienda uchaguzi mkuu hata ukishinda kura zote za wajumbe wote WA mikoa hiyo mingine na zanzibar aliyeshinda dar es salaam ndiye atakuwa Raisi wa NCHI.

CLINTON kwa kura za wananchi alishinda kuwa raisi wa marekani.Lakini kwa kura hizo za kibaguzi za wajumbe wa majimbo tajiri kashindwa na TRUMP.Wangepiga kura kama sisi tunavyopiga Mama CLINTON ndiye angekuwa raisi wa marekani.Marekani mikoa na miji tajiri ndio inaamua nani awe raisi sababu huwa na wajumbe wengi kuliko mikoa na miji maskini.
 
Mleta mada naona uelewi vizuri hiyo Electoral votes inavyofanya kazi. Hao uliowaita wajinga wakipiga kura nyingi na kushinda state/mkoa for that matter ndio wanamwezesha huyo delegate wa electoral vote kupiga kura. Na ndio maana hata Trump kawatumia hao " wajinga" kwenye remote States kupata electoral votes kwa ahadi za maajabu. Kwa taarifa yako ikipigwa popular vote US kuamua kama huo mfumo uendelee au la, unaweza kupigwa chini. Fanya Ref kuanzia uchaguzi wa US kuanzia 2000 utanielewa.
Naona lengo lako pia ni pumba, US walianzisha huo mfumo kuongeza uwiano katika maamuzi kuchagua Rais wao kwenye majimbo, sasa wewe unataka utumike ili eti watu wasio soma wasipige kura...Vipi wewe!
 
Vijana wa ukawa bhana.. MUULIZI Bi Clinton analia mpaka Leo analaani electoral votes .. Zikija hizo CCM itashinda kila mpaka Tanzania ibadili jina
 
Utaratibu wa uchaguzi wa marekani ni wa kishetani.Hauchukulii binadamu wote ni sawa.

Mfano mikoa tajiri ya marekani hupewa uzito mkubwa kuliko mikoa maskini kwenye kura.

wanagawa hivi

DAR ES SALAAM-MKOA UNAPEWA KURA 200
Kigoma unapewa kura 10
LINDI kura 5
Rukwa kura 5
dodoma kura 20
pwani-25
Zanzibar kura 30

Kwa hiyo ukienda uchaguzi mkuu hata ukishinda kura zote za wajumbe wote WA mikoa hiyo mingine na zanzibar aliyeshinda dar es salaam ndiye atakuwa Raisi wa NCHI.

CLINTON kwa kura za wananchi alishinda kuwa raisi wa marekani.Lakini kwa kura hizo za kibaguzi za wajumbe wa majimbo tajiri kashindwa na TRUMP.Wangepiga kura kama sisi tunavyopiga Mama CLINTON ndiye angekuwa raisi wa marekani.Marekani mikoa na miji tajiri ndio inaamua nani awe raisi sabab huwa na wajumbe wengi kuliko mikoa na miji maskini.
MkUu haupo makini hivi Dodoma unawapa kura nyingi kuliko kigoma?yaani waha
unawashushua kuliko magogo?
 
...
...
Kwa mfano, Ukisema Prof. Kitila apige kura kumchagua X AU Y na ukasema mtu kama Lusinde apige kura hiyo hiyo kumchagua kati ya X AU Y ni vitu viwili tofauti kabisa,
...
...
Katika wale wanne halafu mmoja ni kichaa basi huyu uliemtaja mara ya pili anaangukia kwenye kundi la wale wamoja katika wale wanne. Kwa hiyo kura yake ilifaa hata isihesabiwe kabisa, au wakusanywe wawe kumi ndio iwe kura moja
 
Back
Top Bottom