Brigedia Chan-ocha
JF-Expert Member
- Mar 7, 2014
- 1,353
- 2,842
Zina faida sana hizi Electoral Votes, Kwa Tanzania kila Mkoa utapewa idadi yake ya wajumbe (Utaratibu wa kuwapata wajumbe na sifa zao utawekwa kwa mujibu wa Sheria na kwa maridhiano ya wadau wote, Wajumbe hawa ni lazima wawe watu weledi, wasomi, wazalendo na watu Intelligent) Idadi ya wajumbe kwa kila mkoa itategemeana na wingi wa watu kwa kila Mkoa, Kwa mfano, kwa mkoa wa Dar. ambao una idadi kubwa ya watu takribani Zaidi ya milioni 4 utapewa idadi kubwa ya wajumbe, Faida ya kuwa na wajumbe hawa ni kwamba, Watanzania wengi hawajasoma au hawana akili timamu au hawana wanachokijua juu ya Nchi yao kwenye mambo ya UTAWALA, SIASA, UCHUMI nk.
Kwa mfano, Thamani ya kura ya mtu mmoja mmoja inatofautiana sana, kwa mfano, Kura ya msomi kwa mfano, wanafunzi wa vyuo vikuu au watumishi wa Umma au binafsi, profesa au Dr. ni tofauti sana na kura ya mtu ambaye si msomi wala si mtumishi.
Kwa mfano, Ukisema Prof. Kitila apige kura kumchagua X AU Y na ukasema mtu kama Lusinde apige kura hiyo hiyo kumchagua kati ya X AU Y ni vitu viwili tofauti kabisa, hivyo kunahitajika tuwe na Electoral Votes ziwe zinaamua nani Rais baada ya kupiga Popular votes.
Yawezekana matatizo ya watanzania yanasababishwa na kura za wapenda Rushwa wakati wa uchaguzi, watu wasio jielewa, watu waliokata tamaa ya maisha, au Uchama-Uchama, hivyo kuhitaji kura za ziada na muhimu kuamua nani Rais.