MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 81
- 95
Katika chaguzi nyingi za kura za maoni ndani ya CCM, asilimia 60 hadi 80 ya walioshinda wamekuwa ni wale walioanza kampeni miaka 2 hadi 3 kabla ya mchakato kuruhusiwa rasmi na chama. Wamewekeza siyo tu muda, bali pia wamenunua ushawishi ndani ya mfumo wa chama kuanzia ngazi ya mashina hadi mkoa – wakitumia fedha kujiimarisha badala ya utendaji na uwajibikaji.
Hali hii inavuruga misingi ya haki, heshima, na maadili ndani ya chama. Inawavunja moyo wanasiasa wanaojitolea kutumikia wananchi kwa moyo wa kizalendo na uwajibikaji wa kweli.
Ni wakati sasa kwa CCM kuanza kuangalia si tu nani ameshinda kura za maoni, bali ni nani aliyewajibika zaidi kwa jamii, ni nani aliyeonesha uadilifu, uchapakazi, na maadili bila kutegemea fedha wala vitisho.
Huu ndio msingi wa kujenga utamaduni mpya wa siasa safi, ambapo viongozi hawasubiri muda ufike wakiwa na mabegi ya fedha, bali wanatumikia jamii kwa miaka yote – kwa uaminifu na kwa moyo wa kizalendo.
CCM isaidie kuibua viongozi wa mfano, si wamiliki wa rafu/mizengwe au fitina