Kwa ufuatiliaji wangu kwa kadri ya uwezo wangu,nimegundua maovu mengi yaliyobainishwa hasa hasa toka mfumo wa vyama vingi kuanza nchini mwetu.Najua kuna maovu mengi,ila kwa leo nayarejea machache yaliyojitokeza.KWANZA makosa ya kifisadi,rushwa na usainiswaji wa mikataba mibovu.PILI uuzwaji wa kiholela wa raslimali zetu hasa wanyama pori hai na madini yetu.TATU uingizwaji wa bidhaa feki,zenye madhara kwa watumiaji na madawa ya kulevya.Maovu hayo baada ya kubainishwa,huishia kiholela.Tunapoelekea ni wapi??