kweli TANZANIA kuna mtu katuroga na hatorudi kutozindua. Ukiwatilia thread za miaka ya nyuma wadau wa upinzani waliibeza serikali kushindwa kuwachukulia hatua mafisadi. Walisema kinagaubaga kuwa akina manji wameweka serikali mifukoni.
Iweje leo wanashuglikiwa watu wamegeuka tena. Tuna safari ndefu. Muwe na kumbukumbu kuwa JPM hakuwa chaguo la mafisadi toka mwanzo alipochukua formu, ndo maana kamati kuu ilipompitisha mafisadi yalijiunga kutaka kumwangusha.
Sumaye na Lowassa walikua maadui miaka nenda rudi lakini kwa sabb ya maghufuli ilibidi wajiunge kulinda maslah yao. Video zmemuonyesha maghufuli kabla ya kuwa rais akilaumu unyonyaji, na alisema wezi watalimia meno, kwenye kampeni alisisitiza kabisa kuwa lazima mafisadi wakione cha moto.
Issue siyo MANJI,issue hapo ni njia inayotumika kumuadhibu Manji.Manji alifanya kazi chini ya utawala wa CCM na alikuwa backed up na system ya Serikali ya CCM,sasa kama wakuu wa nchi walimbackup halafu unamtafuta Manji hivi ni sahihi kweli??
Na kama Manji amehujumu uchumi basi kesi yake ianze kusikilizwa,tusije tukafika mwisho tukamlipa Manji pesa zaidi ya tulivyodhani tumepata.
Huyu Manji alipewa tender ya kutengeneza nguo za jeshi leo ukimkamata ati kakutwa na nguo za jeshi ni ukichaa kabisa,sasa aliyepewa tender kwanini msikute mabaki ya majora ya nguo za jeshi??
Hivi hizo hisa kwenye TIGO nazo aliziiba toka serikalini au alinunua hisa za tigo zikiwa nje ya Tanzania??Ni uendawazimu kumfilisi mtu ukifikiria unamkomoa Manji kumbe unakomoa watanzania na Taifa kwa ujumla.
Leo unadhani ni Manji kesho zamu yako.Hakuna anayetetea ubadhirifu lakini wote wameshtakiwa??UDA Simon Kisena si ndiyo amehongwa shares kabisa kwa sababu ni home boy?Na anajua namna UDA ilivyouzwa kinyemela je huyo ameguswa??
Na Lugumi je ameishaguswa??Au kwa sababu naye ni Home boy??Chenge je?Tusiangalia watu kwa rangi zao,kama ni kuwashtaki waliohujumu uchumi washtakiwe wote,na kesi zao zifanyike kwa uhuru na haki kusiwe na order kutoka juu.
Tusilipizane visasi vya ujanani tuache ujinga,tuteee haki,hata huyo Manji akiwa masikini leo wewe huwezi kuwa tajiri kwa sababu tu Manji amekuwa masikini.Ni upumbavu wa kiwango cha PhD