Tunachotaka 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunachotaka 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tafakari kali, Oct 27, 2012.

 1. tafakari kali

  tafakari kali JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 16, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Paka 2015 imebaki miaka 2 na miezi 2. Mwaka huo ni mwaka ambao watanzania wanaenda kuchagua chama ambacho kitajenga serikali ambayo inatarajiwa kuleta mabadiliko kisiasa,kiutamaduni na hasa kiuchumi,nasema kuchagua chama kwa kuwa paka sasa katiba haijaruhusu kuwa na mgombea binafsi na kwa tafsiri hii(kama katiba mpya haitotoa ruksa pia)watanzania tutatakiwa kuchagua chama makini chenye watu makini, swali ni CHAMA KIPI CHENYE WATU GANI. Je yaweza kuwa ni ccm? au CHADEMA? Mfano tuseme ccm,swali kwa watu wapi? Je ni hawa hawa ambao leo tunashuhudi chaguzi zake zote zimegubikwa na harufu chafu ya rushwa? Ambacho rais wake wa sasa inasemekana nae amepita kw kutumia pesa za kifisadi za EPA kupitia ile kampun ya kaka yake aliyemtangulia ya KIGODA ambayo hakuna awezaye kuizungumzia kwa ukwapuaji wa pesa toka EPA,nani hasa kutoka jamii hii ya ccm tunayeweza kumwamini? Hawa ambao wanawalinda mafisadi kama yule mwanasheria aliyebariki wizi ktk ununuz wa rada? Yule aliyekuwa na mabilioni aliyoyaita ktk ununuzi wa rada na kuyaita vijisenti?ni nani hasa? Chama hiki hiki ambacho mawaziri wake na wakurugezi wake kwa pamoja wanawauza wanyama poli kama twiga mchana kweupe? Chama ambacho wanaopigania haki wanatekwa na kuteswa vibaya ktk msitu wa mabwe pande? (Sisemi kuwa wote ni wabaya ila hatuwezi kuwakubali kwani mlipo si mahali sahihi).Hapana chama hiki si tunachokitaka WATANZANIA.
  WATANZANIA TUNATAKA CHAMA MAKINI AMBACHO KINAELEWA MATWAKWA YA WATANZANIA NA KUJUA PIA KUWA MATAKWA YAO SI UPEPO WA KISIA, IMANI YETU IPO KWA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA),TUNAWATAKA HAWA SI KWA SABABU NYINGINE ILA KWA KUWA TUNAAMINI KUWA WATAWEZA KUFANYA KAZI TOFAUTI NA HAWA ccm,ambao ni wez wanaoiba mchana kweupe na waongo. TUNATAKA KUJENGA UTAMADUNI AMBAO WATU TUKIJUA KUWA TUNAIBIWA BASI TUNAWATOA KUPITIA SANDUKU LA KURA. Kamwe hatutakiwi kurudi nyuma tumesha amka. Tunawaambia ccm kuwa jiandaeni kuwa chama cha upinzani.
  *wenzagu mnasemaje?*
   
 2. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono hoja, ccm imechakaa tubadilishe utawala tuone. Chadema ndo tumaini jipya.
   
Loading...