Kwani wao kufikisha 30+ bila ndoa ni akili au wanajifariji? sawa wanapata wanachokitaka ila wako tofauti sana na waliooa. Ndo maana wanakaa vijiweni badala ya kutafuta maisha. Watoto watazaa na mwisho siku watatakiwa kuoa. watakaa wapi kila siku kumeendea dinner au lunch wa waliooa? Kimya kimya wanawatamani wenye wake zao.
aiseeeee
Yeah ni kwli kabisa nyumba kubwa tena katika kutoa maamuzi hawapewi nafasi maana wanawachukulia kama hamzao.Watu wengi wakiongelea ndoa wanafikiria ni wanawake tu ndio wanapata stress...kuna wanaume nawajua hadi nawahurumia...maana hawatengwi na jamii ila wanajitenga kwa kujishuku...unakuta mtu wadogo zake wana wake yeye akienda kwenye sherehe za familia anakuwa mnyonge sana...oeni vijana...hata nyie umri ukisonga mtachizika...
Ndoa/kuoa ni stage ya mwisho....kufanalize mambo....ni ishara ya mwisho ya upendo,kama unampenda mtu,utataka u spend the rest of your life with,kama unampenda mtu utamjali na kumuheshimu....nyie mnaokuja na mada za kukejeli wanawake,you have never been in love,you dont know the feeling of being in love!sitashangaa kama you are coming from dysfunctional homes!yes km baba yako hakumheshimu mama yako kwa kutembea na kimada chances you will do the same!....ndio nyie mnaokuja hapa women this,women that....hatuwashangai wazee wenu hawakuwafunza kuwa RESPECTFUL TO WOMEN....
Jana baada ya kutoka kazini nilienda kijiweni kubadilishana mawazo na vijana wenzangu,
Miongoni mwa vijana waliokuwepo pale kuna vijana umri umeenda wana kama 30+ lakini hawajaoa na mada iliyokuwepo mezani ni ndoa za siku hizi na kwanini vijana wanaogopa kuoa, vijana wale wakanijibu kuwa kwanini waoe wakati wakihitaji tendo hata kila siku toka kwa wapenzi wao wanapata na hata watoto wanaweza pata toka kwa wapenzi bila kuwaoa, nimefikria maneno hayo nimegundua wanawake/wasichana ndo wana matatizo maana wanajirahisi mno na kutumika mno kwa wapenzi mwisho wa siku wanaachwa bila ndoa haiwezekani kila siku unatumika halafu uolewe mtaishia kuchezewa na kuachwa na mkumbuke vimezaliwa vingi vya utamu na mkichezewa mkishaona mnazeeka mnaanza stress zenu na kulazimisha ndoa kumbe mlichezea usichana wenu.
hovyoooo.