Tuna viongozi ambao wamelala usingizi wa pono

Tuna viongozi ambao wamelala usingizi wa pono

JackisonDubai

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2023
Posts
537
Reaction score
1,285
MBONA SIELEWI?

Tuna uhuru lakini hatupo huru.
Hatujafungwa kamba lakini haturuhusiwi kusogea.
Tunaruhusiwa kukaa vikao tu sio kujadili.
Tunaruhusiwa kuwaza sio kuamua.
Tumepewa viongozi sio waongozaji.
Tunaweza kusoma na kufaulu sio kufanikiwa.
Tuna Uhuru wa kuongea sio kusikilizwa.
Mbaya si mkosaji ni mkosoaji.
Mwerevu sio mfichuaji ni mfichaji.

Kicheko cha mnyonge huitwa hatari kwa taifa lakini mkubwa akiua inaitwa kulinda Amani. Waliopo mbele wamesimama wa nyuma wamekaa lakini wanasema wote tunaona sinema.

Tupo pamoja lakini tembo upande ule na swala kuleee nyuma. Magoli yanahesabiwa kabla ya mchezo na ushindi unapangwa sio unatafutwa.

Kama maisha ndio hivi ngoja nirudi darasani nikajifunze maana ya kupewa UHURU na KUWA HURU.
Ameandika Baba Mchungaji Jason Kahembe
 
Back
Top Bottom