Tuna uhakika kuwa eMALALAMIKO si avantra?

Tuna uhakika kuwa eMALALAMIKO si avantra?

Mohamed Abubakar

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2014
Posts
1,127
Reaction score
1,290
Nauliza hivi nikitaka ufafanuzi iwapo kuna yyt aliyewahi kutumia emamamiko kupata mrejesho wowote.

Nani ni msimamizi wa mtandao huu.

Nani kawahi kupata mrejesho kutokana na malalamiko na kero za ufanisi wa watendaji wa Serikali.

Na mwisho baada ya kutoa malalamiko nimemtumia ujumbe ule ule niliotumiwa mwaka haja kuwa nanukuu...

Mpendwa xxxxx xxxxxx lalamiko lako namba yyyyyy limeshajibiwa na MOHA.

Aidha kwa ufuatiliaji wa awali katika Ofisi ya Msajili imebainika kuwa majibu ya maombi yenu yapo kwenye hatua za mwisho za uchakataji hivyo majibu hayo yanaweza kuwasilishwa kwenu kupitia mfumo wa RSMIS ndani ya week mbili kutoka sasa.

Tafadhali endeleeni kuangalia katika akaunti yenu mliyotumia kutuma maombi.

Tunashukuru kwa ushirikiano wako.

Suali langu je ni message kama hii imeandikwa na binadamu. Kama ni binadamu kwanini hawajibiki.

Kwanini maneno ni yaleyale hakuna uwajibikaji.

Kwangu naona ni mzaha na matumizi ya fujo ya pesa za walipa kodi.

Pia soma >> eMALALAMIKO: Mfumo huu wa kuwasilisha malalamiko serikalini utatekeleza majukumu kusudiwa?
 
Ni mfumo huo, ukute hata hawana habari kama uliwatumia ujumbe. Serikalini baadhi ya watu wanastrago kupata ajira, wakiingia ajirani wanaanza kusaka passwords za WIFI ili wachati na kuona umbeaumbea mitandaoni. Pole sana.
 
Back
Top Bottom