Tuna Jambo la kujifunza hapa

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
FUTURE OF ENGLAND IS IN SAFE HANDS!

Naam km wanavyosema waswahili,km unataka kesho yako iwe nzuri basi anza kuitengeneza Leo na nyumba huwa huanzi kuezeka mabati Bali utaanzia na msingi hii ndio imebeba dhamana ya post yangu hii kuhusu wajukuu Wa malkia ukipenda Waite "The three lions"...

Tunaanzia hapaa hivi.. Ujerumani baada yakufeli sana kwenye WC 2006 iliofanyika nyumbani kwao pmj na Euro2008 huku kikosi kikiwa ni kilekile basi waliamua kuanza upya kusuka timu ambayo waliplan ije kutisha kwa miaka ijayo wala hawakuangalia kwa wakati ule naongelea mwaka2009 hap vilisukwa vikosi vingi vya vijana ila ntagusia cha German U21 iliundwa na baadhi ya watu km Manuel Neuer,Muller,Hummels,Boateng,Ozil,khedira,Howedes,Marin, Marcel shmelzer nk na huku German U17 ikuundwa na watu km Marc Ter Stegen,Beno Leno,Mustaphi,Mario Gotze,Can Emre, nk baada ya miaka(6) ujerumani ilienda kubeba WC pale Brazil yote n matunda ya project hii na ikumbukwe jinsi ilivyokua tishio mpk kupewa jina LA German machine kwa visago vilivyokua vinatembea basi turudi hapa kwa England...

Kwa wenye kumbukumbu nzuri watakumbuka jinsi England ilivyofeli pale south Africa bila kusahau Brazil kule pia ikumbukwe kile kikosi chao cha U21 kilivyofanywa kitu kibaya mwaka2013 kwenye Euro U21 kwa kumaliza kundi na point0 kikosi kile kilichokua na baadhi ya watu kina Dany Rose,Zaha,Tom Ince,Josh McEachrain,Redmond,Clyne,Jordan Henderson walitia aibu kubwa na inasemekana viongozi Wa FA walienda kupata baadhi ya mafunzo kwa wenzao Wa DFB(chama cha soka German) England nao waliamua kuwekeza upya kwenye soka la vijana na matunda yake yameanza kuonekana hivi sasa...

Unakumbuka kile kikosi cha England U17 kilichobeba kombe la dunia la vijana mwaka2017? Basi km huwakumbuki ndio hawa hapa waliounda kikosi kile "Steven sessegnon,Mark Guehi,George McEachran(mdogo Wa Josh), Phil Phoden( mchezaji bora),Emil Smith Rowe,Cullum Hudson Odoi,Jadon Sancho,Angel Gomes,Rhian Brewster(Top score), Morgan Gibbs-white nk

Je unakijua kikosi chao kilichoshiriki Euro U21 mwaka2019?? Unajua kitachofuata n nn na plan yao hawa? Unajua kwann walimuamini kocha wao alianzia na vijana km german walivyomuani joachim low?? Basi Itaendelea..nikipata Mda maana mda wangu ni mchache cm yakugongea ila tupo pamoja waungwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya Mwisho...
FUTURE OF ENGLAND IS IN SAFE HANDS

Sifa kubwa ya England siku zote ni majivuno haswa yanatengenezwaga na wandishi wahabari wao pale timu yao ya Taifa inapoenda kushiriki mashindano yoyote ya mataifa km unakumbukumbu kile kikosi chao cha dhahabu kilivyokua kinapigiwa promo kila kona ya dunia lkn hakuna chamaana walichofanya nii hvyo hvyo waliwapigia promo vijana wao wale wa mwaka2013 waliotia aibu kwenye Euro championship U21 wenzao km Spain kulikua na watu sana km kina De Gea,Alcantara,Isco,Ilarramendi,koke,Morata,Carvajal,Nacho, Sarabia nk, huko uholanzi wakiwa na vichwa km Blind, de vrij,strootman,Wijnaldum,Classie,Indi,Van Ginkel utaona apo ilikua n mbingu na ardhi kina Hendo nawenzake Redmond sio wakucompare na hio miamba walistahili walichokipata,

Ila matumaini ya wajukuu wa malkia yamerudi upya haswa ni hawa vijana waliobeba World cup U17 mwaka 2017 kwa kuifunga Spain mabao 5:2 na chakufurajisha zaidi asilimia 70% yakile kikosi cha wale vijana wanapata nafasi Mara kibao kwenye vilabu vyao nawaongelea zaidi Jadon Sancho, Phil Phoden,Hudson Odoi,Ryan Sessegnon,Morgan Gibbs White, pia kina Emil Smith Rowe mara kadhaa hupata nafasi pale Arsenal, Angel Gomes pia Rhian Brewster wa Liverpool ila kuna kilabu ya championship Mara kadhaa namuonaga sikumbuki jina pia Marc Guehi & Conor Callagher(Chelsea)

IPO hivi target ya waingereza ni World cup 2022 kule Qatar na vijana wao watakua maturity zaidi nawaongelea kiumri ifakopo mwaka huo...
Dean Henderson(25), dele Alli(25)James Madison(25),Joe Gomes(24),Rashford(24),Abraham(24),Mason Mount(23),Trent Arnold (23),Phoden,Sancho, Odoi,Sessegnon, Smith Rowe wote(21)!!
Apo kuna vichwa km Wan Bissaka,Ben Chilwell,Holgate,Jack Grealish,Gray,Reece James,Declan Rice,Tomori kina Dominic Calvert lewin,Harvey Barnes,Clarke salter n.k na wote hawa asilimia 90% ni first eleven kwenye vilabu vyao tena Big team kabisa mkiona lampard anajaza na kuwakumbatia watoto wakingereza msibeze wanayo ajenda yao kumbuka ni mmoja wapo wawale kikosi cha dhahabu kilichofeli vibaya!

Bado watakuwepo watu km Hary Maguire,Stones,Sterling, Kane, na wengineo huyu kocha wao Southgate wachezaji wengi kwasasa alianza nao timu za vijana wenzetu wanawekeza kuanzia mbali APA kunamfano wakuiga kwetu pia hakuna njia za mkato kufikia huko!!
Naam naweza kusema sasa Future ya Three lions IPO katika mikono salama kabisa mda utongea

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom