Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,618
Viongozi wetu wa Afrika wanapaswa kujifunza kwa wenzao waliowatangulia mambo mengi sana.
Ungemwambia Mugabe ile mwezi wa Tisa mwaka jana kuwa atakuwa chini ya ulinzi na wananchi watabeba mabango ya kumwambia aondoke angeliagiza ufungwe miaka 10. Lakini ndani ya wiki moja tu akiwa chini ya ulinzi wananchi wanapiga Selfie na wanajeshi huko njee na kuvua nguo zao kuwafuta boot zao vumbi.
Gadafi ungemwambia kuwa siku ya kuuawawa kwake angelitolewa ndani ya mtaro wa maji taka akiwa amejificha kama panya angelikufukuza Libya au angekikufunga zaidi ya nusu Karne au hata kukuua kabisa. Lakini wakati anakamatwa alikuwa peke yake wapambe wake wote waliokuwa wanakunywa na kujenga mahema pindi wanaposafiri walikuwa wameachana naye. Gadafi anakamatwa na vijana wadogo na kumburuza chini huku akivumilia soli za boot za waandamanaji waliokuwa wanamkanyaga usoni.
Mubaraki kule Misri ungemwambia angekamatwa na kushatakiwa kipindi kile akiwa kwenye ubora wake angekufunga au kukufukuza Misri. Ilianza kiutani kwa waandamanaji kujitokoze na kusema hawamtaki tena, akatuma majeshi yake badala ya kuwafukuza waandamanaji wakawa wanapiga nao selfie wananchi.
Gbagbo Kule Ivory Coast alikuwa haamini kilichokuwa kinatokea siku ya kukamatwa kwake. Alipigwa vibao na wanajeshi mbele ya mke wake huku mkewe akifanyiwa vitendo vya Kinyama kabisa. Wapo wengi wa Kutolea mfano ila tunajifunza nn haswa katika haya?
KWA VIONGOZI WETU.
#Jambo la Msingi kabisa la Kujifunza ni kutokuamini wananchi mnaowaongoza. Kelele zao uwapo jukwaani, kukushangilia uwapo Jukwaani, Urafiki ulionao na baadhi ya unaowazunguka na kukuaminisha kuwa wewe ndio wewe, wapambe wote wanaokusifu na kukuleta habari mbalimbali na hata mlinzi wako sio watu wa kuamini hata kidogo.
Mugabe alizomewe na kudhihakiwa kwenye nchi aliyokuwa akishangiliwa na kuonekana kama kiongozi Shujaa. Hawa waliomdhihaki hawajakodishwa nje ya nchi ya Zimbabwe hapana hawa ni wale wale waliokuwa wanamshangilia.
Hawa wanaobeba Mabango Leo pale Kampala ni wale wale waliokuwa wanamshangilia Museven wakati hali ikiwa Tulivu.
Hizi Tweet za Kina Trump na media za njee zinazochochea ni zile zile zilizokuwa zinamsifu wakati mabepari wakitaka Shaba na Mafuta ya Uganda.
NINI WAKIFANYE VIONGOZI WETU?
Kwanza kabisa wamshukuru Mungu kwa kuwapa Nafasi walizonazo. Hili ni la msingi sana na wakati wakiwa katika ubora wao wakumbuke ipo siku watachoka na itawapasa kuwaachia wengine waendelee walipoishia.
Wafanye yale ambayo siku ambayo hawatakuwa na madaraka basi wanaweza kujichanganya na wananchi wengine na kunywa kikombe cha kahawa kwa pamoja. Hakuna furaha kama utastaafu halafu watu wakawa na hamu ya kukaa na wewe na kuzungumza na wewe nk.
Baada ya kustaafu Mwl Nyerere aliendelea kutoa hutuba zilizopendwa na mahali alipoitwa kuhutubia watu walifurika na kumsikiliza. Si viongozi wote wanaoweza kuishi maisha aliyoishi Mwl Nyerere njee ya Uongozi.
Waliopo madarakani kuna cha Kujifunza hapa.