Tuna hitaji kudai uhuru kwa mara ya pili. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuna hitaji kudai uhuru kwa mara ya pili.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MwanaFalsafa1, May 23, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ndugu Watanzania, tuna hitaji kudai uhuru tena! Siyo uhuru wa kuji tawala wa Tanganyika wa mwaka 1961 au wa Zanzibar wa mwaka 1963 bali uhuru wa kiuchumi, Economic Independence. Kwani tulipo dai uhuru wa kuji tawala bila kujiandaa na uhuru wa kiuchumi aidha kwa kuto kujua au kwa kupuuza tuli kuwa hatuja pata uhuru kamili na matokeo yake yanaonekana hadi leo. Wakoloni walijua na kuliona hilo, sisi hatukuona.

  Kwabla sija endelea kuongelea kuhusu Tanzania ngoja nitoe mfano. Mfano wenyewe ni Afrika Kusini. Afrika kusini kwa miaka mingi ilidai kuvunjwa kwa serikali ya makaburu. Wakadai haki sawa na wenzao wa kizungu. Mwaka 1994 waka pewa na kwa mara ya kwanza serikali iliongozwa na weusi. Lakini hadi leo hii weusi walio kuwa wanadai usawa hawaoni mabadiliko yoyote licha ya kuji tawala. Kwa nini? Ni kwa sababu japo kwenye serikali wao ndiyo walio wengi lakini wanao shikilia uchumi bado ni weupe. matokeo yake ni kwamba licha ya kuji tawala bado weusi wana jiona kwenye hali ile ile ya kimaisha waliyo kuwa nayo wakati wa utawala wa kibaguzi.

  Wenzangu kwa kizungu hali yetu inaitwa neo colonialism au indirect rule. Ukoloni mambo leo una tokana na ukweli kwamba bado hatuja shika vyanzo vyetu vya uchumi na bado tuna tegemea misaada ya wale wale tulio "wafukuza". Tokea lini mtu aliye kutawala kimabavu aka taka kukusaidia bila kuwa na faida yoyote kwake? Leo hii tuna tawaliwa na nchi wakopeshaji na mashirika mbali mbali ya kifeha ya kimataifa kama IMF na WB. Nchi hizi na mashirika haya kabla ya kutoa "misaada" wana toa "mapendekezo" ya mabadiliko ya kisera kwenye uchumi na biashara. Mabadiliko haya mara zote ni yale yanayo lenga kuwa nufaisha wao kibiashara au kiutawala. Kwa kifupi weka sheria tunazo taka sisi au msaada haupati. Hivyo ndivyo tunvyo tawaliwa kwenye karne ya ishirini na moja. Wanajua fika kwa vile tuna :jitawala" wenyewe basi sera wata kazo ziweka lawama ita bebwa na serikali ya wananchi wetu wenyewe.

  Nchi nyingi za Afrika zime pata uhuru muda sawa na zile za Asia kama Indonesia nk. Wakati wa kupata uhuru Indonesia na Kenya zilikua na uchumi karibia sawa. Leo hii hauwezi kulinganisha Indonesia na Kenya kwenye kipengele chochote. Kwa nini wenzetu waliweza sisi tuka shindwa mpaka leo hii tuna baki tegemezi? Ni kwa sababu wenzetu wali subutu. Walijua uhuru wa kuji tawala una kuja bega kwa bega na uhuru wa kiuchumi. Hauwezi ukawa na moja uka kosa nyingine uka jiita huru. Tume kuwa kama watoto wadogo ambao tunaogopa kutembea kwa hiyo tunaendelea kumshika mama atukinge. Tunaogopa kwamba tuki jaribu kutembea wenyewe basi tuta dondoka na kuchubuka bila kujua kwamba kabla ya kuweza kutembea ni lazima tuumie. Tume kuwa kama kijana aliye fikia umri wa kuji tegemea lakini kwa kuogopa majukumu tunaendelea kuishi kwenye nyumba ya wazazi. Matokeo yake ni nini? Matokeo ni kuendelea kuishi chini ya sheria na masharti ya "baba" na "mama" kwa kuogopa kufukuzwa nyumbani. Ni lini tuta ona kwamba tume kuwa na tuna hitaji kuji tegemea sasa? Ni lini tutaendelea kuishi chini ya paa la wazazi ambao sisi tuna waita wazungu?

  Sasa ni wakati wa serikali kuamka. Ni wakati wa viongozi kutambua kwamba mtu anaye kopa siku zote haishiwi na deni bali ana kata pua kuunga wajihi. Ni wakati sasa Tanzania ikawa nchi inayo jitegemea ili tuweze kweli kuji tawala na kujiamulia mambo yetu. Sawa mwanzo tuta dondoka na kuchubuka! Sawa mwanzo hatuta ishi maisha kama tuliyo kuwa tukiishi chini ya "wazazi". Mwanzo siku zote ni mgumu lakini hakika tunaweza. Ina sikitisha, ina huzunisha na ina katisha tamaa. Nchi yenye rasilimali na utajiri kama wetu kuendelea kuitwa nchi "masikini" ni aibu. ufike wakati tuone haya sasa. Uhuru wa kweli, uhuru wa kuji tawala una tokana na uhuru wa kiuchumi. Ni hayo tu wakuu.
   
Loading...