Nyakabindione
Member
- Jan 5, 2015
- 7
- 1
TUMWACHE JPM APUMZIKE
Taifa lilipatwa na msiba mzito tarehe 17 Machi 2021 kwa kupotelewa na kiongozi wake shupavu, Rais wa Awamu ya Tano Dkt John Pombe Joseph Magufuli. Kwa hakika, huu ni msiba mzito kwa taifa. Ni msiba mzito kwa sababu haijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu rais aliyeko madarakani kufariki dunia. Ni ukweli usiopingika kwamba taifa lilitikisika pale msiba ulipotangazwa na aliyekuwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hasaan.
Baada ya kutangazwa msiba huo mzito, kuliibuka makundi mawili miongoni mwa Watanzania. Hilo halifichiki. Kuna kundi lililonesha 'kushangilia' msiba huu. Na kuna lile lililonesha 'kuomboleza' msiba huu. Maandishi yangu hayatajikita kuangalia sababu za haya makundi kushangilia na/au kuomboleza kwa wakati mmoja. Maandishi yangu yatajikita kuyaomba au kuyaasa makundi haya KUMWACHA JPM APUMZIKE.
Kwa nini naandika kuyaomba makundi haya KUMWACHA JPM APUMZIKE? Ninawiwa kuandika hivyo kwani kadri siku zinavyokwenda, majibizano ya makundi haya nayo yanaongezeka. Ripoti ya CAG nayo kwa namna moja imekuja kuongeza majibizano haya. Wapo waliofikia kumtuhumu mpaka CAG kwamba ripoti yake ni ya uongo na kwamba imeandaliwa mahsusi kumchafua JPM. Hii siyo halali kabisa. Hatumtendei haki marehemu.
Iko wazi, kama binadamu JPM alitenda mambo mbalimbali. Yapo mazuri, yapo mabaya pia. Mazuri yaliwafurahisha wote au wengi. Mioyo yao ilinawiri na kupata bashasha. Mabaya yaliwakasirisha walioguswa. Yapo mabaya pia yaliyowaumiza watu na watu wao. Mioyo yao ikaumia, nafsi zao zikakasirika na kusinyaa. Ni sehemu ya ubinadamu wake.
Wakati nasoma Kidato cha Pili, mwalimu wangu wa Fizikia alinifundisha Newton's Laws of Motion tatu. Kuna ya kwanza, ya pili na ya tatu. Kanuni ya tatu inasema, "To every action, there's an equal and opposite reaction". Sina uhakika kama nimeinukuu kwa usahihi. Lakini lengo langu hapa ni kutumia maudhui yake tu katika mjadala wangu. Kwa tafsiri isiyo rasmi, "Kwa kila tendo, kuna mwitikio ulio sawa au ulio kinyume na tendo husika". Mtu ukimpa mkate naye atakupa juisi. Lakini ukimpa konzi, naye atakupa kofi!
Kwa wale tunaomthamini marehemu JPM tuwe wa kwanza kumtakia mapumziko mema. Mazuri yake yanajulikana na yanaonekana. Hayahitaji kuhubiriwa. Tunapozidi kuyaandika mtandaoni au hata kuyasimulia kwenye vyombo vya habari, tunatonesha vidonda vya wale walioumia, waliokasirika na kusinyaa mioyo. Tuyaache mazuri yake yajitangaze yenyewe ili kuwaziba midomo pia wanaoandika au kusimulia mabaya yake. Kwa kufanya hivi, tutakuwa tumemtendea haki marehemu. Haki yake ya kupumzika.
R. I. P JPM.